Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Umetoa maagizo yako ili tuyatii kwa ukamilifu.

  2. Laiti mwenendo wangu ungekuwa imara katika kuyatii maagizo yako!

  3. Hivyo mimi sitaaibishwa ninapozingatia amri zako zote.

  4. Nitakusifu kwa moyo mnyofu ninapojifunza sheria zako za haki.

  5. Nitayatii maagizo yako; usiniache kabisa.

  6. Kijana aifanye njia yake kuwa safi jinsi gani? Ni kwa kutii, akilifuata neno lako.

  7. Ninakutafuta kwa moyo wangu wote, usiniache niende mbali na amri zako.

  8. Nimelificha neno lako moyoni mwangu ili nisikutende dhambi.

  9. Sifa ni zako, Ee Bwana, nifundishe maagizo yako.

  10. Kwa midomo yangu nitasimulia sheria zote zinazotoka katika kinywa chako.

  11. Ninafurahia kufuata sheria zako kama mtu afurahiaye mali nyingi.

  12. Ninatafakari maagizo yako na kuziangalia njia zako.

  13. Ninafurahia maagizo yako, wala sitalipuuza neno lako.

  14. Mtendee mema mtumishi wako, nami nitaishi; nitalitii neno lako.

  15. Yafungue macho yangu nipate kuona mambo ya ajabu katika sheria yako.

  16. Mimi ni mgeni duniani, usinifiche amri zako.

  17. Nafsi yangu inataabika kwa shauku kubwa juu ya sheria zako wakati wote.

  18. Unawakemea wenye majivuno, waliolaaniwa waendao mbali na amri zako.

  19. Niondolee dharau na dhihaka, kwa kuwa ninazishika sheria zako.

  20. Ingawa watawala huketi pamoja na kunisingizia, mtumishi wako atatafakari juu ya maagizo yako.

  21. Nimelazwa chini mavumbini, yahifadhi maisha yangu sawasawa na neno lako.

  22. Nilikueleza njia zangu ukanijibu, nifundishe sheria zako.

  23. Nijulishe mafundisho ya mausia yako, nami nitatafakari maajabu yako.

  24. Nafsi yangu imechakazwa kwa huzuni, uniimarishe sawasawa na neno lako.

  25. Niepushe na njia za udanganyifu, kwa neema unifundishe sheria zako.