Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Nimechagua njia ya kweli, nimekaza moyo wangu katika sheria zako.

  2. Nimengʼangʼania sheria zako, Ee Bwana, usiniache niaibishwe.

  3. Nakimbilia katika njia ya maagizo yako, kwa kuwa umeuweka moyo wangu huru.

  4. Ee Bwana, nifundishe kuyafuata maagizo yako, nami nitayashika mpaka mwisho.

  5. Nipe ufahamu, nami nitaishika sheria yako na kuitii kwa moyo wangu wote.

  6. Niongoze kwenye njia ya amri zako, kwa kuwa huko napata furaha.

  7. Ugeuze moyo wangu kuelekea sheria zako, na siyo kwenye mambo ya ubinafsi.

  8. Geuza macho yangu kutoka kwenye mambo yasiyofaa, uyahifadhi maisha yangu sawasawa na neno lako.

  9. Mtimizie mtumishi wako ahadi yako, ili upate kuogopwa.

  10. Niondolee aibu ninayoiogopa, kwa kuwa sheria zako ni njema.

  11. Tazama jinsi ninavyoonea shauku mausia yako! Hifadhi maisha yangu katika haki yako.

  12. Ee Bwana, upendo wako usiokoma unijie, wokovu wako sawasawa na ahadi yako,

  13. ndipo nitakapomjibu anayenidhihaki, kwa kuwa ninalitumainia neno lako.

  14. Usilinyakue neno la kweli kutoka kinywani mwangu, kwa kuwa nimeweka tumaini langu katika amri zako.

  15. Nitaitii amri yako daima, naam, milele na milele.

  16. Nitatembea nikiwa huru, kwa kuwa nimejifunza mausia yako.

  17. Nitasema sheria zako mbele za wafalme wala sitaaibishwa,

  18. kwa kuwa ninazifurahia amri zako kwa sababu ninazipenda.

  19. Ninaziinulia amri zako ambazo ninazipenda mikono yangu, nami ninatafakari juu ya maagizo yako.

  20. Kumbuka neno lako kwa mtumishi wako, kwa sababu umenipa tumaini.

  21. Faraja yangu katika mateso yangu ni hii: Ahadi yako inahifadhi maisha yangu.

  22. Wenye majivuno wamenisimanga bila kuchoka, hata hivyo sitaiacha sheria yako.

  23. Ee Bwana, ninazikumbuka sheria zako za zamani, nazo zinanifariji.

  24. Nimeshikwa sana na ghadhabu kwa ajili ya waovu, ambao wameacha sheria yako.

  25. Ee Bwana, wakati wa usiku ninalikumbuka jina lako, nami nitatii sheria yako.