Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Nafsi yangu inazimia kwa kutamani wokovu wako, lakini nimeweka tumaini langu katika neno lako.

  2. Macho yangu yamefifia, nikingoja ahadi yako; ninasema, “Utanifajiri lini?”

  3. Ingawa nimekuwa kama kiriba kwenye moshi, bado sijasahau maagizo yako.

  4. Mtumishi wako itampasa angoje mpaka lini? Ni lini utawaadhibu washtaki wangu?

  5. Wenye majivuno wananichimbia mashimo, kinyume na sheria yako.

  6. Amri zako zote ni za kuaminika; unisaidie, kwa sababu watu wananishtaki bila sababu.

  7. Walikaribia kabisa kunifuta kutoka uso wa dunia, lakini sijaacha mausia yako.

  8. Yahifadhi maisha yangu sawasawa na upendo wako, nami nitatii sheria za kinywa chako.

  9. Ee Bwana, neno lako ni la milele, linasimama imara mbinguni.

  10. Uaminifu wako unaendelea kwa vizazi vyote, umeiumba dunia, nayo inadumu.

  11. Sheria zako zinadumu hadi leo, kwa kuwa vitu vyote vinakutumikia.

  12. Kama nisingefurahia sheria yako, ningeangamia katika taabu zangu.

  13. Sitasahau mausia yako kamwe, kwa maana kwayo umehifadhi maisha yangu.

  14. Uniokoe, kwa maana mimi ni wako, kwa kuwa nimetafuta mausia yako.

  15. Waovu wanangojea kuniangamiza, bali mimi ninatafakari sheria zako.

  16. Katika ukamilifu wote ninaona mna kikomo, lakini amri zako hazina mpaka.

  17. Aha! Tazama, sheria yako naipenda mno ajabu. Ninaitafakari mchana kutwa.

  18. Amri zako zimenipa hekima zaidi kuliko adui zangu, kwa kuwa nimezishika daima.

  19. Nina akili zaidi kuliko walimu wangu wote, kwa kuwa ninatafakari juu ya sheria zako.

  20. Nina ufahamu zaidi kuliko wazee, kwa kuwa ninayatii mausia yako.

  21. Nimezuia miguu yangu isiende kwenye kila njia mbaya, ili niweze kutii neno lako.

  22. Sijaziacha sheria zako, kwa kuwa umenifundisha wewe mwenyewe.

  23. Tazama jinsi maneno yako yalivyo matamu kwangu, matamu kuliko asali katika kinywa changu!

  24. Ninapata ufahamu kutoka mausia yako, kwa hiyo ninachukia kila njia ya upotovu.

  25. Nimeapa na nimethibitisha, kwamba nitafuata sheria zako za haki.