God
Mistari inayomtaja God
Nimeteseka sana, uhifadhi maisha yangu, Ee Bwana, sawasawa na neno lako.
Ee Bwana, pokea sifa za hiari za kinywa changu, nifundishe sheria zako.
Ingawa maisha yangu yako hatarini siku zote, sitasahau sheria yako.
Waovu wamenitegea mtego, lakini sijayakiuka maagizo yako.
Nimekusudia moyoni mwangu kuyafuata maagizo yako mpaka mwisho.
Ninachukia watu wa nia mbili, lakini ninapenda sheria yako.
Wewe ni kimbilio langu na ngao yangu, nimeweka tumaini langu katika neno lako.
Ondokeni kwangu, ninyi mtendao mabaya, ili niweze kushika amri za Mungu wangu!
Nihifadhi sawasawa na ahadi yako, nami nitaishi; usiache matumaini yangu yakavunjwa.
Nitegemeze, nami nitaokolewa, nami daima nitayaheshimu maagizo yako.
Unawakataa wote wanaoyaasi maagizo yako, kwa maana udanganyifu wao ni bure.
Waovu wa nchi unawatupa kama takataka, kwa hivyo nazipenda sheria zako.
Mwili wangu unatetemeka kwa kukuogopa wewe, ninaziogopa sheria zako.
Mhakikishie mtumishi wako usalama, usiache wenye kiburi wanionee.
Macho yangu yamefifia, yakitazamia wokovu wako, na kuitazamia ahadi yako ya kweli.
Mfanyie mtumishi wako kulingana na upendo wako na unifundishe maagizo yako.
Mimi ni mtumishi wako; nipe ufahamu ili niweze kuelewa sheria zako.
Ee Bwana, wakati wako wa kutenda umewadia, kwa kuwa sheria yako inavunjwa.
Kwa sababu nazipenda amri zako zaidi ya dhahabu, naam, zaidi ya dhahabu safi,
na kwa sababu naona maagizo yako yote ni adili, nachukia kila njia potovu.
Kuingia kwa maneno yako kunaleta nuru, kunampa mjinga ufahamu.
Nimefungua kinywa changu na kuhema, nikitamani amri zako.
Nigeukie na unihurumie, kama uwafanyiavyo siku zote wale wanaolipenda jina lako.
Ongoza hatua zangu kulingana na neno lako, usiache dhambi yoyote initawale.
Niokoe na uonevu wa wanadamu, ili niweze kutii mausia yako.