Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Hili limekuwa zoezi langu: nami ninayatii mausia yako.

  2. Ee Bwana, wewe ni fungu langu, nimeahidi kuyatii maneno yako.

  3. Nimetafuta uso wako kwa moyo wangu wote, nihurumie sawasawa na ahadi yako.

  4. Nimezifikiri njia zangu na nimeelekeza hatua zangu katika mausia yako.

  5. Nitafanya haraka bila kuchelewa kuzitii amri zako.

  6. Hata waovu wanifunge kwa kamba, sitasahau sheria yako.

  7. Usiku wa manane ninaamka kukushukuru kwa sababu ya sheria zako za haki.

  8. Mimi ni rafiki kwa wale wote wakuchao, kwa wote wanaofuata mausia yako.

  9. Ee Bwana, dunia imejaa upendo wako, nifundishe maagizo yako.

  10. Mtendee wema mtumishi wako Ee Bwana, sawasawa na neno lako.

  11. Nifundishe maarifa na uamuzi mzuri, kwa kuwa ninaamini amri zako.

  12. Kabla sijapata shida nilipotea njia, lakini sasa ninalitii neno lako.

  13. Wewe ni mwema, unalotenda ni jema, nifundishe maagizo yako.

  14. Ingawa wenye majivuno wamenisingizia uongo, nitafuata mausia yako kwa moyo wangu wote.

  15. Mioyo yao ni katili na migumu, bali mimi napendezwa na sheria yako.

  16. Ilikuwa vyema mimi kupata shida ili nipate kujifunza maagizo yako.

  17. Sheria inayotoka kinywani mwako ina thamani kubwa kwangu kuliko maelfu ya vipande vya fedha na dhahabu.

  18. Mikono yako ilinifanya na kuniumba, nipe ufahamu niweze kujifunza amri zako.

  19. Wakuchao wafurahie wanaponiona, kwa kuwa nimeweka tumaini langu katika neno lako.

  20. Ee Bwana, ninajua kwamba sheria zako ni za haki, katika uaminifu wako umeniadhibu.

  21. Upendo wako usiokoma uwe faraja yangu, sawasawa na ahadi yako kwa mtumishi wako.

  22. Huruma yako na inijie ili nipate kuishi, kwa kuwa naifurahia sheria yako.

  23. Wenye majivuno na waaibishwe kwa kunikosea mimi bila sababu, lakini mimi nitatafakari juu ya mausia yako.

  24. Wale wakuchao na wanigeukie mimi, hao ambao wanazielewa sheria zako.

  25. Moyo wangu usiwe na lawama katika kutii maagizo yako, ili nisiaibishwe.