Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Mkononi mwa Bwana kuna kikombe kilichojaa mvinyo unaotoka povu uliochanganywa na vikolezo; huumimina, nao waovu wote wa dunia hunywa mpaka tone la mwisho.

  2. Bali mimi, nitatangaza hili milele; nitaimba sifa kwa Mungu wa Yakobo.

  3. Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Zaburi ya Asafu. Wimbo. Katika Yuda, Mungu anajulikana, jina lake ni kuu katika Israeli.

  4. Hema lake liko Salemu, makao yake katika Sayuni.

  5. Huko alivunja mishale imetametayo, ngao na panga, silaha za vita.

  6. Kwa kukemea kwako, Ee Mungu wa Yakobo, farasi na gari la vita vilikaa kimya.

  7. Wewe peke yako ndiye wa kuogopwa. Ni nani awezaye kusimama mbele yako unapokasirika?

  8. wakati wewe, Ee Mungu, ulipoinuka kuhukumu, kuwaokoa wote walioonewa katika nchi.

  9. Hakika ghadhabu yako dhidi ya wanadamu inakuletea sifa, na masalia ya ghadhabu yako unajifunga mshipi.

  10. Wekeni nadhiri kwa Bwana Mungu wenu na kuzitimiza; nchi zote za jirani na walete zawadi kwa Yule astahiliye kuogopwa.

  11. Huvunja roho za watawala; anaogopwa na wafalme wa dunia.

  12. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Asafu. Nilimlilia Mungu ili anisaidie, nilimlilia Mungu ili anisikie.

  13. Nilipokuwa katika taabu, nilimtafuta Bwana, usiku nilinyoosha mikono bila kuchoka na nafsi yangu ilikataa kufarijika.

  14. Ee Mungu, nilikukumbuka wewe, nikalia kwa huzuni; nikatafakari, roho yangu ikadhoofika.

  15. “Je, Bwana atakataa milele? Je, hatatenda mema tena?

  16. Je, upendo wake usio na mwisho umetoweka milele? Je, ahadi yake imekoma nyakati zote?

  17. Je, Mungu amesahau kuwa na huruma? Je, katika hasira amezuia huruma yake?”

  18. Ndipo nikawaza, “Huu ndio udhaifu wangu: lakini nitakumbuka miaka ya mkono wa kuume wa Aliye Juu Sana.”

  19. Nitayakumbuka matendo ya Bwana; naam, nitaikumbuka miujiza yako ya zamani.

  20. Nitazitafakari kazi zako zote na kuyawaza matendo yako makuu.

  21. Ee Mungu, njia zako ni takatifu. Ni mungu yupi aliye mkuu kama Mungu wetu?

  22. Wewe ndiwe Mungu utendaye miujiza, umeonyesha uwezo wako katikati ya mataifa.

  23. Kwa mkono wako wenye nguvu umewakomboa watu wako, uzao wa Yakobo na Yosefu.

  24. Maji yalikuona, Ee Mungu, maji yalikuona yakakimbia, vilindi vilitetemeka.

  25. Mawingu yalimwaga maji, mbingu zikatoa ngurumo kwa radi, mishale yako ikametameta huku na huko.