Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Ee Bwana Mwenyezi, nitakuja na kutangaza matendo yako makuu, nitatangaza haki yako, yako peke yako.

  2. Ee Mungu, umenifundisha tangu ujana wangu, hadi leo ninatangaza matendo yako ya ajabu.

  3. Ee Mungu, usiniache, hata niwapo mzee wa mvi, mpaka nitangaze uwezo wako kwa kizazi kijacho, nguvu zako kwa wote watakaokuja baadaye.

  4. Ee Mungu, haki yako imefika juu katika mbingu, wewe ambaye umefanya mambo makuu. Ee Mungu, ni nani aliye kama wewe?

  5. Ee Mungu wangu, nitakusifu kwa kinubi kwa ajili ya uaminifu wako; Ee Uliye Mtakatifu wa Israeli, nitakuimbia sifa kwa zeze.

  6. Midomo yangu itapaza sauti kwa furaha ninapokuimbia sifa, mimi, ambaye umenikomboa.

  7. Ulimi wangu utasimulia matendo yako ya haki mchana kutwa, kwa maana wale waliotaka kunidhuru, wameaibishwa na kufadhaishwa.

  8. Zaburi ya Solomoni. Ee Mungu, mjalie mfalme aamue kwa haki yako, mwana wa mfalme kwa haki yako.

  9. Atawaamua watu wako kwa haki, watu wako walioonewa kwa haki.

  10. Atawatetea walioonewa miongoni mwa watu na atawaokoa watoto wa wahitaji, ataponda mdhalimu.

  11. Atadumu kama jua lidumuvyo, kama mwezi, vizazi vyote.

  12. Jina lake na lidumu milele, na lidumu kama jua. Mataifa yote yatabarikiwa kupitia kwake, nao watamwita aliyebarikiwa.

  13. Bwana Mungu, Mungu wa Israeli, apewe sifa, yeye ambaye peke yake hutenda mambo ya ajabu.

  14. Jina lake tukufu lisifiwe milele, ulimwengu wote ujae utukufu wake.

  15. Zaburi ya Asafu. Hakika Mungu ni mwema kwa Israeli, kwa wale ambao mioyo yao ni safi.

  16. Kwa hiyo watu wao huwageukia na kunywa maji tele.

  17. Wanasema, “Mungu awezaje kujua? Je, Yeye Aliye Juu Sana anayo maarifa?”

  18. Mpaka nilipoingia patakatifu pa Mungu, ndipo nilipotambua mwisho wao.

  19. Hakika unawaweka mahali pa utelezi, unawaangusha chini kwa uharibifu.

  20. Kama ndoto mtu aamkapo, hivyo wakati uinukapo, Ee Bwana, utawatowesha kama ndoto.

  21. nilikuwa mpumbavu na mjinga, nilikuwa mnyama mkatili mbele yako.

  22. Hata hivyo niko pamoja nawe siku zote, umenishika mkono wangu wa kuume.

  23. Unaniongoza kwa shauri lako, hatimaye utaniingiza katika utukufu.

  24. Nani niliye naye mbinguni ila wewe? Dunia haina chochote ninachokitamani ila wewe.

  25. Mwili na moyo wangu vyaweza kushindwa, bali Mungu ni nguvu ya moyo wangu na fungu langu milele.