Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Sifa apewe Bwana, Mungu Mwokozi wetu, ambaye siku kwa siku hutuchukulia mizigo yetu.

  2. Mungu wetu ni Mungu aokoaye, Bwana Mwenyezi hutuokoa na kifo.

  3. Hakika Mungu ataponda vichwa vya adui zake, vichwa vya hao waendao katika njia za dhambi.

  4. Bwana alisema, “Nitawarudisha kutoka Bashani; nitawarudisha kutoka vilindi vya bahari,

  5. Ee Mungu, maandamano yako yameonekana, maandamano ya Mungu wangu, Mfalme wangu, yakielekea patakatifu pake.

  6. Msifuni Mungu katika kusanyiko kubwa, msifuni Bwana katika kusanyiko la Israeli.

  7. Ee Mungu, amuru uwezo wako, Ee Mungu tuonyeshe nguvu zako, kama ulivyofanya hapo awali.

  8. Kwa sababu ya Hekalu lako Yerusalemu wafalme watakuletea zawadi.

  9. Mkemee mnyama aliyeko kwenye manyasi, kundi la mafahali katikati ya ndama za mataifa. Na walete minara ya madini ya fedha wakinyenyekea. Tawanya mataifa yapendayo vita.

  10. Wajumbe watakuja kutoka Misri, Kushi atajisalimisha kwa Mungu.

  11. Mwimbieni Mungu, enyi falme za dunia, mwimbieni Bwana sifa,

  12. mwimbieni sifa yeye apandaye mbingu za kale zilizo juu, yeye angurumaye kwa sauti kuu.

  13. Tangazeni uwezo wa Mungu, ambaye fahari yake iko juu ya Israeli, ambaye uwezo wake uko katika anga.

  14. Ee Mungu, wewe unatisha katika mahali patakatifu pako, Mungu wa Israeli huwapa watu wake uwezo na nguvu. Mungu Asifiwe!

  15. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Yungiyungi.” Zaburi ya Daudi. Ee Mungu, niokoe, kwa maana maji yamenifika shingoni.

  16. Nimechoka kwa kuomba msaada, koo langu limekauka. Macho yangu yanafifia, nikimtafuta Mungu wangu.

  17. Ee Mungu, wewe unajua upumbavu wangu, wala hatia yangu haikufichika kwako.

  18. Ee Bwana, ewe Bwana Mwenye Nguvu Zote, wakutumainio wasiaibishwe kwa ajili yangu; wakutafutao wasifedheheshwe kwa ajili yangu, Ee Mungu wa Israeli.

  19. Kwa maana nimestahimili dharau kwa ajili yako, aibu imefunika uso wangu.

  20. Kwa kuwa wivu wa nyumba yako unanila, matukano ya wale wanaokutukana yameniangukia.

  21. Lakini Ee Bwana, ninakuomba, kwa wakati ukupendezao; katika upendo wako mkuu, Ee Mungu, unijibu kwa wokovu wako wa hakika.

  22. Ee Bwana, unijibu, kwa wema wa upendo wako; kwa huruma zako nyingi unigeukie.

  23. Usimfiche mtumishi wako uso wako, uharakishe kunijibu, kwa sababu niko katika shida.

  24. Unajua jinsi ninavyodharauliwa, kufedheheshwa na kuaibishwa, adui zangu wote unawajua.

  25. Uwamwagie ghadhabu yako, hasira yako kali na iwapate.