God
Mistari inayomtaja God
Kwa kuwa wanawatesa wale uliowajeruhi, na kuzungumza juu ya maumivu ya wale uliowaumiza.
Walipize uovu juu ya uovu, usiwaache washiriki katika wokovu wako.
Mimi niko katika maumivu na dhiki; Ee Mungu, wokovu wako na unihifadhi.
Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo, nami nitamtukuza kwa kumtolea shukrani.
Hili litampendeza Bwana kuliko ngʼombe dume, zaidi ya fahali akiwa na pembe na kwato zake.
Maskini wataona na kufurahi: ninyi mnaomtafuta Mungu, mioyo yenu na iishi!
Bwana huwasikia wahitaji wala hadharau watu wake waliotekwa.
Mbingu na dunia zimsifu, bahari na vyote viendavyo ndani yake,
kwa maana Mungu ataiokoa Sayuni na kuijenga tena miji ya Yuda. Kisha watu watafanya makao yao humo na kuimiliki,
watoto wa watumishi wake watairithi na wale wote walipendao jina lake wataishi humo.
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Maombi. Ee Mungu, ufanye haraka kuniokoa; Ee Bwana, njoo hima unisaidie.
Lakini wote wakutafutao washangilie na kukufurahia, wale wapendao wokovu wako siku zote waseme, “Mungu na atukuzwe!”
Lakini bado mimi ni maskini na mhitaji; Ee Mungu, unijie haraka. Wewe ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu; Ee Bwana, usikawie.
Ee Bwana, nimekukimbilia wewe, usiache nikaaibika kamwe.
Kwa haki yako uniponye na kuniokoa, unitegee sikio lako uniokoe.
Uwe kwangu mwamba wa kimbilio, mahali nitakapokimbilia kila wakati; toa amri ya kuniokoa, kwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu.
Ee Mungu wangu uniokoe kutoka kwenye mkono wa mwovu, kutoka kwenye makucha ya watu wabaya na wakatili.
Kwa kuwa umekuwa tumaini langu, Ee Bwana Mwenyezi, tegemeo langu tangu ujana wangu.
Tangu kuzaliwa nimekutegemea wewe, ulinitoa tumboni mwa mama yangu. Nitakusifu wewe daima.
Nimekuwa kama kioja kwa wengi, lakini wewe ni kimbilio langu imara.
Kinywa changu kimejazwa sifa zako, nikitangaza utukufu wako mchana kutwa.
Wanasema, “Mungu amemwacha, mkimbilieni mkamkamate, kwani hakuna wa kumwokoa.”
Ee Mungu, usiwe mbali nami, njoo haraka kunisaidia, Ee Mungu wangu.
Lakini mimi, nitatumaini siku zote, nitakusifu zaidi na zaidi.
Kinywa changu kitasimulia haki yako, wokovu wako mchana kutwa, ingawa sifahamu kipimo chake.