Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Wale walio mbali nawe wataangamia, unawaangamiza wote wasio waaminifu kwako.

  2. Lakini kwangu mimi, ni vyema kuwa karibu na Mungu. Nimemfanya Bwana Mwenyezi kimbilio langu; nami nitayasimulia matendo yako yote.

  3. Utenzi wa Asafu. Ee Mungu, mbona umetukataa milele? Mbona hasira yako inatoka moshi juu ya kondoo wa malisho yako?

  4. Kumbuka watu uliowanunua zamani, kabila la urithi wako, ambao uliwakomboa: Mlima Sayuni, ambamo uliishi.

  5. Geuza hatua zako kuelekea magofu haya ya kudumu, uharibifu wote huu ambao adui ameuleta pale patakatifu.

  6. Adui zako wamenguruma pale ulipokutana nasi, wanaweka bendera zao kama alama.

  7. Waliteketeza kabisa mahali pako patakatifu, wakayanajisi makao ya Jina lako.

  8. Walisema mioyoni mwao, “Tutawaponda kabisa!” Walichoma kila mahali ambapo Mungu aliabudiwa katika nchi.

  9. Ee Mungu, mtesi atakudhihaki mpaka lini? Je, adui watalitukana jina lako milele?

  10. Kwa nini unazuia mkono wako, mkono wako wa kuume? Uutoe kutoka makunjo ya vazi lako na uwaangamize!

  11. Lakini wewe, Ee Mungu, ni mfalme wangu tangu zamani, unaleta wokovu duniani.

  12. Ni wewe uliyeigawanya bahari kwa uweza wako; ulivunja vichwa vya wanyama wakubwa wa kutisha katika maji.

  13. Ni wewe uliyefungua chemchemi na vijito, ulikausha mito ambayo ilikuwa ikitiririka daima.

  14. Mchana ni wako, nao usiku ni wako pia, uliziweka jua na mwezi.

  15. Ni wewe uliyeiweka mipaka yote ya dunia, ulifanya kiangazi na masika.

  16. Ee Bwana, kumbuka jinsi mtesi alivyokudhihaki, jinsi watu wapumbavu walivyolitukana jina lako.

  17. Usiukabidhi uhai wa njiwa wako kwa wanyama wakali wa mwitu; usisahau kabisa uhai wa watu wako wanaoteseka milele.

  18. Usiruhusu walioonewa warudi nyuma kwa aibu; maskini na wahitaji hebu walisifu jina lako.

  19. Inuka, Ee Mungu, ujitetee; kumbuka jinsi wapumbavu wanavyokudhihaki mchana kutwa.

  20. Usipuuze makelele ya watesi wako, ghasia za adui zako, zinazoinuka mfululizo.

  21. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu!” Zaburi ya Asafu. Wimbo. Ee Mungu, tunakushukuru, tunakushukuru wewe, kwa kuwa jina lako li karibu; watu husimulia matendo yako ya ajabu.

  22. Unasema, “Ninachagua wakati maalum; ni mimi nihukumuye kwa haki.

  23. Wakati dunia na watu wake wote inapotetemeka, ni mimi ninayezishikilia nguzo zake imara.

  24. Kwa wale wenye majivuno ninasema, ‘Msijisifu tena,’ kwa wale waovu, ‘Msiinue pembe zenu.

  25. Bali Mungu ndiye ahukumuye: Humshusha huyu na kumkweza mwingine.