Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Kwa hiyo akamaliza siku zao katika ubatili na miaka yao katika vitisho.

  2. Kila mara Mungu alipowaua baadhi yao, waliosalia walimtafuta, walimgeukia tena kwa shauku.

  3. Walikumbuka kwamba Mungu alikuwa Mwamba wao, kwamba Mungu Aliye Juu Sana alikuwa Mkombozi wao.

  4. Lakini walimdanganya kwa vinywa vyao, wakisema uongo kwa ndimi zao,

  5. mioyo yao haikuwa thabiti kwake, wala hawakuwa waaminifu katika agano lake.

  6. Hata hivyo alikuwa na huruma, alisamehe maovu yao na hakuwaangamiza. Mara kwa mara alizuia hasira yake, wala hakuchochea ghadhabu yake yote.

  7. Alikumbuka kwamba wao walikuwa nyama tu, upepo upitao ambao haurudi.

  8. Mara ngapi walimwasi jangwani na kumhuzunisha nyikani!

  9. Walimjaribu Mungu mara kwa mara, wakamkasirisha yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.

  10. Hawakukumbuka uwezo wake, siku aliyowakomboa kutoka kwa mtesi,

  11. siku aliyoonyesha ishara zake za ajabu huko Misri, maajabu yake huko Soani.

  12. Aliwafungulia hasira yake kali, ghadhabu yake, hasira na uadui, na kundi la malaika wa kuharibu.

  13. Aliitengenezea njia hasira yake, hakuwaepusha na kifo, bali aliwaachia tauni.

  14. Lakini aliwatoa watu wake kama kundi, akawaongoza kama kondoo kupitia jangwani.

  15. Aliwaongoza salama, wala hawakuogopa, bali bahari iliwameza adui zao.

  16. Hivyo akawaleta hadi kwenye mpaka wa nchi yake takatifu, hadi nchi ya vilima ambayo mkono wake wa kuume ulikuwa umeitwaa.

  17. Lakini wao walimjaribu Mungu, na kuasi dhidi ya Yeye Aliye Juu Sana, wala hawakuzishika sheria zake.

  18. Wakamkasirisha Mungu kwa mahali pao pa juu pa kuabudia miungu, wakachochea wivu wake kwa sanamu zao.

  19. Wakati Mungu alipowasikia, alikasirika sana, akamkataa Israeli kabisa.

  20. Akaiacha hema ya Shilo, hema aliyokuwa ameiweka katikati ya wanadamu.

  21. Akalipeleka Sanduku la nguvu zake utumwani, utukufu wake mikononi mwa adui.

  22. Aliachia watu wake wauawe kwa upanga, akaukasirikia sana urithi wake.

  23. Ndipo Bwana alipoamka kama vile kuamka usingizini, kama vile mtu aamkavyo kutoka kwenye bumbuazi la mvinyo.

  24. Aliwapiga na kuwashinda adui zake, akawatia katika aibu ya milele.

  25. Ndipo alipozikataa hema za Yosefu, hakulichagua kabila la Efraimu,