Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Widow

62 mistari · 5 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Umewafukuza wajane mikono mitupu na kuzivunja nguvu za yatima.

  2. Huwanyangʼanya yatima punda wao, na kumchukua rehani fahali wa mjane.

  3. Huwafanya mawindo wanawake tasa na wasio na watoto, nao hawaonyeshi huruma kwa wajane.

  4. Mtu aliyekuwa karibu kufa alinibariki, nami niliufanya moyo wa mjane kuimba.

  5. “Ikiwa nimewanyima maskini haja zao, au kuyaacha macho ya wajane yadhoofike,

  6. basi mkono wangu na unyofoke toka begani mwangu, nao na uvunjike kutoka kiungio chake.

  7. Baba wa yatima, mtetezi wa wajane, ni Mungu katika makao yake matakatifu.

  8. Wanamchinja mjane na mgeni, na kuwaua yatima.

  9. Bwana huwalinda wageni na kuwategemeza yatima na wajane, lakini hupinga njia za waovu.

  10. Bwana hubomoa nyumba ya mtu mwenye kiburi, bali huilinda mipaka ya mjane isiguswe.

  11. jifunzeni kutenda mema! Tafuteni haki, watieni moyo walioonewa. Teteeni shauri la yatima, wateteeni wajane.

  12. Watawala wenu ni waasi, rafiki wa wevi, wote wanapenda rushwa na kukimbilia hongo. Hawatetei yatima, shauri la mjane haliletwi mbele yao lisikilizwe.

  13. Ole wao wawekao sheria zisizo za haki, kwa wale watoao amri za kuonea,

  14. kuwanyima maskini haki zao na kuzuilia haki za watu wangu walioonewa, kuwafanya wajane mawindo yao na kuwanyangʼanya yatima.

  15. kama msipomwonea mgeni, yatima wala mjane, na kumwaga damu isiyo na hatia mahali hapa, nanyi kama msipofuata miungu mingine kwa madhara yenu wenyewe,

  16. ndipo nitawaacha mkae mahali hapa, katika nchi niliyowapa baba zenu milele na milele.

  17. Hili ndilo Bwana asemalo: Tenda haki na adili. Mwokoe mkononi mwa mdhalimu yeye aliyetekwa nyara. Usimtendee mabaya wala ukatili mgeni, yatima au mjane, wala usimwage damu isiyo na hatia mahali hapa.

  18. Waache yatima wako; nitayalinda maisha yao. Wajane wako pia wanaweza kunitumaini mimi.”

  19. Ndani yako wamewadharau baba na mama, ndani yako wamewatendea wageni udhalimu na kuwaonea yatima na wajane.

  20. Msimwonee mjane wala yatima, mgeni wala maskini. Msiwaziane mabaya mioyoni mwenu ninyi kwa ninyi.’

  21. “Basi nitakuja karibu nanyi ili kuhukumu. Nami nitakuwa mwepesi kushuhudia dhidi ya wachawi, wazinzi, waapao kwa uongo, wanaopunja vibarua malipo yao, wanaowaonea wajane na yatima, na wanaowanyima wageni haki, lakini hawaniogopi mimi,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

  22. Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, enyi wanafiki! Mnakula katika nyumba za wajane, nanyi kwa kujifanya kuwa wema, mnasali sala ndefu. Kwa hiyo hukumu yenu itakuwa kuu zaidi.]

  23. Wao hula nyumba za wajane, na ili waonekane kuwa wema wanasali sala ndefu. Watu kama hawa watapata hukumu iliyo kuu sana.”

  24. Wao hula nyumba za wajane, na ili waonekane kuwa wema, wanasali sala ndefu. Watu kama hawa watapata hukumu iliyo kuu sana.”

  25. Hivyo basi, kama huyo mwanamke ataolewa na mwanaume mwingine wakati mumewe akiwa bado yuko hai, ataitwa mzinzi. Lakini kama mumewe akifa, mwanamke huyo hafungwi tena na sheria ya ndoa, naye akiolewa na mtu mwingine haitwi mzinzi.