Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Wicked

724 mistari · 18 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Mpumbavu hufurahia tabia mbaya, lakini mtu mwenye ufahamu hupendezwa na hekima.

  2. Kile anachoogopa mwovu ndicho kitakachompata; kile anachoonea shauku mwenye haki atapewa.

  3. Tufani inapopita, waovu hutoweka, lakini wenye haki husimama imara milele.

  4. Tarajio la mwenye haki ni furaha, bali matumaini ya mwovu huwa si kitu.

  5. Njia ya Bwana ni kimbilio kwa wenye haki, lakini ni maangamizi ya wale watendao mabaya.

  6. Kamwe wenye haki hawataondolewa, bali waovu hawatasalia katika nchi.

  7. Midomo ya wenye haki inajua kile kinachofaa, bali kinywa cha mwovu hujua kile kilichopotoka tu.

  8. Uadilifu wa wenye haki huwaongoza, bali wasio waaminifu huharibiwa na hila yao.

  9. Haki ya wasio na lawama, huwatengenezea njia iliyonyooka, bali waovu huangushwa kwa uovu wao wenyewe.

  10. Haki ya wanyofu huwaokoa, bali wasio waaminifu hunaswa na tamaa mbaya.

  11. Mtu mwenye haki huokolewa kutoka taabu, naye mtu mwovu huingia humo badala yake.

  12. Wakati mwenye haki anapofanikiwa, mji hufurahi; mwovu atowekapo, kuna kelele za furaha.

  13. Kutokana na baraka ya mtu mnyofu mji hukwezwa, bali kwa kinywa cha mwovu mji huharibiwa.

  14. Mtu mwovu hupata ujira wa udanganyifu, bali yeye apandaye haki huvuna tuzo ya uhakika.

  15. Mtu mwenye haki kweli kweli hupata uzima, bali yeye afuatiliaye ubaya huendea kifo chake.

  16. Bwana huwachukia sana watu wenye moyo wa upotovu, bali hupendezwa na wale ambao njia zao hazina lawama.

  17. Uwe na hakika na hili: Waovu hawataepuka kuadhibiwa, bali wenye haki watakuwa huru.

  18. Shauku ya mwenye haki huishia tu kwenye mema, bali tumaini la mwovu huishia tu kwenye ghadhabu.

  19. Kama wenye haki watapokea ujira wao duniani, si zaidi sana yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi?

  20. Mtu hathibitiki kutokana na uovu, bali mwenye haki hataondolewa.

  21. Mipango ya mtu mwadilifu ni ya haki, bali ushauri wa mwovu ni udanganyifu.

  22. Maneno ya waovu huotea kumwaga damu, bali maneno ya waadilifu huwaokoa.

  23. Watu waovu huondolewa na kutoweka, bali nyumba ya mwenye haki husimama imara.

  24. Mtu mwovu hunaswa kwa mazungumzo yake ya dhambi, bali mwenye haki huepuka taabu.

  25. Hakuna dhara linalompata mwenye haki, bali waovu wana taabu nyingi.