Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Uprightness

60 mistari · 55 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Anahifadhi ushindi kwa ajili ya mwadilifu, yeye ni ngao kwa wale wasio na lawama,

  2. wale waachao mapito yaliyonyooka wakatembea katika njia za giza,

  3. Kwa maana wanyofu wataishi katika nchi, nao wasio na lawama watabakia ndani yake.

  4. Mtu mwadilifu hutembea salama, lakini mtu aendaye katika njia zilizopotoka atagunduliwa.

  5. Njia ya Bwana ni kimbilio kwa wenye haki, lakini ni maangamizi ya wale watendao mabaya.

  6. Uadilifu wa wenye haki huwaongoza, bali wasio waaminifu huharibiwa na hila yao.

  7. Haki ya wanyofu huwaokoa, bali wasio waaminifu hunaswa na tamaa mbaya.

  8. Kutokana na baraka ya mtu mnyofu mji hukwezwa, bali kwa kinywa cha mwovu mji huharibiwa.

  9. Bwana huwachukia sana watu wenye moyo wa upotovu, bali hupendezwa na wale ambao njia zao hazina lawama.

  10. Maneno ya waovu huotea kumwaga damu, bali maneno ya waadilifu huwaokoa.

  11. Haki humlinda mtu mwadilifu, bali uovu humwangusha mwenye dhambi.

  12. Yeye ambaye njia zake ni nyofu humcha Bwana, bali yeye ambaye njia zake zimepotoka humdharau Mungu.

  13. Nyumba ya mwovu itaangamizwa, bali hema la mnyofu litastawi.

  14. Bwana huchukia sana dhabihu za waovu, bali maombi ya wanyofu humfurahisha Mungu.

  15. Upumbavu humfurahisha mtu ambaye hana akili, bali mtu mwenye ufahamu hushika njia iliyonyooka.

  16. Njia kuu ya wanyofu huepuka ubaya; yeye aichungaye njia yake, huchunga maisha yake.

  17. Afadhali mtu maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama, kuliko mpumbavu ambaye midomo yake imepotoka.

  18. Mtu mwovu ana uso wa ushupavu, bali mtu mnyofu huzifikiria njia zake.

  19. Afadhali maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama kuliko tajiri ambaye njia zake ni potovu.

  20. Yeye ambaye humwongoza mwenye haki kwenye mapito mabaya, ataanguka kwenye mtego wake mwenyewe, bali wasio na lawama watapokea urithi mwema.

  21. Yeye ambaye mwenendo wake hauna lawama hulindwa salama, bali yeye ambaye njia zake ni potovu ataanguka ghafula.

  22. Watu wamwagao damu humchukia mtu mwadilifu na hutafuta kumuua mtu mnyofu.

  23. Kama mtu akimdekeza mtumishi wake tangu ujanani, atamletea sikitiko mwishoni.

  24. Hili ndilo peke yake nililolipata: Mungu amemuumba mwanadamu mnyofu, lakini mwanadamu amebuni mambo mengi.”

  25. Nichukue twende nawe, na tufanye haraka! Mfalme na anilete ndani ya vyumba vyake. Marafiki Tunakushangilia na kukufurahia, tutasifu upendo wako zaidi kuliko divai. Mpendwa Tazama jinsi ilivyo bora wakupende!