Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Uprightness

60 mistari · 55 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Ninajua, Mungu wangu, kwamba wewe huujaribu moyo na unapendezwa na unyofu. Vitu hivi vyote nimetoa kwa hiari na kwa moyo mnyofu. Nami sasa nimeona kwa furaha jinsi watu wako walioko hapa kwa hiari yao walivyokutolea wewe.

  2. Lakini makuhani walikuwa wachache sana kuweza kuchuna wale wanyama wote wa sadaka za kuteketezwa, kwa hiyo ndugu zao Walawi wakawasaidia mpaka kazi ile ikakamilika na mpaka makuhani wengine walipowekwa wakfu, kwa kuwa Walawi walikuwa makini kujiweka wakfu kuliko walivyokuwa makuhani.

  3. ikiwa wewe ni safi na mnyofu, hata sasa atainuka mwenyewe kwa niaba yako, na kukurudisha katika mahali pako pa haki.

  4. “Nimekuwa mtu wa kuchekwa na rafiki zangu, ingawa nilimwita Mungu naye akanijibu: mimi ni mtu wa kuchekwa tu, ingawa ni mwadilifu na nisiye na hatia!

  5. Kwa kuwa Bwana ni mwenye haki, yeye hupenda haki. Wanyofu watauona uso wake.

  6. Ni yule aendaye pasipo mawaa, atendaye yaliyo haki, asemaye kweli toka moyoni mwake,

  7. Nimekuwa sina hatia mbele zake, nami nimejilinda nisitende dhambi.

  8. Bwana amenilipa sawasawa na uadilifu wangu; sawasawa na usafi wa mikono yangu machoni pake.

  9. Mlinde mtumishi wako na dhambi za makusudi, nazo zisinitawale. Ndipo nitakapokuwa sina lawama, wala sitakuwa na hatia ya kosa kubwa.

  10. Bali mimi ninaishi maisha yasiyo na lawama; nikomboe na unihurumie.

  11. Mwimbieni Bwana kwa furaha, enyi wenye haki; kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo.

  12. Waovu huchomoa upanga na kupinda upinde, ili wawaangushe maskini na wahitaji, kuwachinja wale ambao njia zao ni nyofu.

  13. Bwana anazifahamu siku za wanyofu, na urithi wao utadumu milele.

  14. Watafakari watu wasio na hatia, wachunguze watu wakamilifu, kuna mafanikio kwa mtu apendaye amani.

  15. Katika uadilifu wangu unanitegemeza na kuniweka kwenye uwepo wako milele.

  16. Kama kondoo, wamewekewa kwenda kaburini, nacho kifo kitawala. Wanyofu watawatawala asubuhi, maumbile yao yataozea kaburini, mbali na majumba yao makubwa ya fahari.

  17. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu!” Utenzi wa Daudi. Enyi watawala, je, kweli mwanena kwa haki? Je, mnahukumu kwa unyofu miongoni mwa watu?

  18. Unasema, “Ninachagua wakati maalum; ni mimi nihukumuye kwa haki.

  19. Naye Daudi aliwachunga kwa uadilifu wa moyo, kwa mikono ya ustadi aliwaongoza.

  20. Kwa kuwa Bwana ni jua na ngao, Bwana hutoa wema na heshima; hakuna kitu chema anachowanyima wale ambao hawana hatia.

  21. Msifuni Bwana. Nitamtukuza Bwana kwa moyo wangu wote, katika baraza la wanyofu na katika kusanyiko.

  22. Watoto wake watakuwa wenye uwezo katika nchi, kizazi cha watu waadilifu kitabarikiwa.

  23. Hata gizani nuru humzukia mtu mwadilifu, yule mwenye rehema, huruma na haki.

  24. Ee Bwana, watendee mema walio wema, wale walio wanyofu wa moyo.

  25. Hakika wenye haki watalisifu jina lako, na waadilifu wataishi mbele zako.