Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu The Miracles of Christ

193 mistari · 30 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Yesu akawajibu, “Huyu mtu wala wazazi wake hawakutenda dhambi. Alizaliwa kipofu ili kazi za Mungu zidhihirishwe katika maisha yake.

  2. Yanipasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenituma wakati bado ni mchana, kwa kuwa usiku waja ambapo hakuna mtu awezaye kufanya kazi.

  3. Wakati niko ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu.”

  4. Baada ya kusema haya, akatema mate ardhini, akatengeneza tope kwa mate na kumpaka yule mtu kipofu machoni.

  5. Kisha akamwambia, “Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu.” (Siloamu maana yake ni aliyetumwa.) Ndipo yule kipofu akaenda, akanawa, naye akarudi akiwa anaona.

  6. Hakuna mtu aniondoleaye uhai wangu, bali ninautoa kwa hiari yangu mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa uhai wangu na pia ninao uwezo wa kuutwaa tena. Amri hii nimepewa na Baba yangu.”

  7. Baada ya kusema haya, Yesu akawaambia, “Rafiki yetu Lazaro amelala, lakini naenda kumwamsha.”

  8. Wanafunzi wakamwambia, “Bwana, kama amelala usingizi ataamka.”

  9. Hata hivyo, Yesu alikuwa anazungumzia kuwa Lazaro amekufa, lakini wanafunzi wake hawakuelewa, walidhani kwamba anasema Lazaro amelala usingizi tu.

  10. Kwa hiyo Yesu akawaambia waziwazi, “Lazaro amekufa.

  11. Hata hivyo nafurahi kwa kuwa sikuwepo huko kabla ya Lazaro kufa, ili mpate kuamini. Lakini sasa twendeni kwake.”

  12. Tomaso aliyeitwa Pacha akawaambia wanafunzi wenzake, “Sisi nasi twendeni tukafe pamoja naye.”

  13. Yesu alipowasili huko alikuta Lazaro amekuwa kaburini siku nne.

  14. Basi Bethania ulikuwa karibu na Yerusalemu umbali wa karibu maili mbili,

  15. na Wayahudi wengi walikuwa wamekuja kuwafariji Martha na Maria kwa ajili ya kufiwa na ndugu yao.

  16. Martha aliposikia kwamba Yesu anakuja, alitoka kwenda kumlaki, ila Maria alibaki nyumbani.

  17. Martha akamwambia Yesu, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, ndugu yangu hangalikufa.

  18. Lakini sasa ninajua kuwa chochote utakachomwomba Mungu, atakupa.”

  19. Yesu akamwambia, “Ndugu yako atafufuka.”

  20. Martha akamjibu, “Ninajua ya kuwa atafufuka wakati wa ufufuo wa wafu siku ya mwisho.”

  21. Yesu akamwambia, “Mimi ndiye huo ufufuo na uzima. Yeye aniaminiye mimi, hata akifa atakuwa anaishi

  22. na yeyote aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je, unasadiki haya?”

  23. Martha akamwambia, “Ndiyo Bwana, ninaamini ya kuwa wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yeye ajaye ulimwenguni.”

  24. Baada ya kusema haya Martha alikwenda, akamwita Maria dada yake faraghani na kumwambia, “Mwalimu yuko hapa anakuita.”

  25. Maria aliposikia hivyo, akaondoka upesi akaenda mpaka alipokuwa Yesu.