Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu The Jews: Abraham

7 mistari · 158 vipengele

Mistari kuhusu Abraham

  1. Bwana akawa amemwambia Abramu, “Ondoka kutoka nchi yako, uache jamii yako na nyumba ya baba yako, uende hadi nchi nitakayokuonyesha.

  2. “Mimi nitakufanya taifa kubwa na nitakubariki, Nitalikuza jina lako, nawe utakuwa baraka.

  3. Nitawabariki wale wanaokubariki, na yeyote akulaaniye nitamlaani; na kupitia kwako mataifa yote duniani yatabarikiwa.”

  4. Baada ya Loti kuondoka Bwana akamwambia Abramu, “Ukiwa hapo ulipo, inua macho yako utazame kaskazini na kusini, mashariki na magharibi.

  5. Nchi yote unayoiona nitakupa wewe na uzao wako hata milele.

  6. Nitaufanya uzao wako uwe mwingi kama mavumbi ya nchi, hivyo kama kuna yeyote awezaye kuhesabu mavumbi, basi uzao wako utahesabika.

  7. Ondoka, tembea katika marefu na mapana ya nchi, kwa maana ninakupa wewe.”