Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Tabernacle: Pattern of, revealed to Moses

7 mistari · 94 vipengele

Mistari kuhusu Pattern of, revealed to Moses

  1. Tengeneza hema hili na vyombo vyake vyote sawasawa na kielelezo nitakachokuonyesha.

  2. “Simamisha Hema sawasawa na mfano ulioonyeshwa kule mlimani.

  3. Kwa hiyo kazi yote ya maskani, Hema la Kukutania ikakamilika. Waisraeli wakafanya kila kitu sawasawa kama vile Bwana alivyomwagiza Mose.

  4. Waisraeli walikuwa wamefanya kazi yote sawasawa na vile Bwana alivyokuwa amemwagiza Mose.

  5. Mose akakagua kazi na kuona kuwa walikuwa wameifanya sawasawa kama vile Bwana alivyokuwa ameagiza. Kwa hiyo Mose akawabariki.

  6. “Baba zetu walikuwa na lile Hema la Ushuhuda huko jangwani. Lilikuwa limetengenezwa kama Mungu alivyokuwa amemwelekeza Mose, kulingana na kielelezo alichoona.

  7. Wanahudumu katika patakatifu palipo mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni. Hii ndiyo sababu Mose alionywa alipokaribia kujenga hema, akiambiwa: “Hakikisha kuwa unavitengeneza vitu vyote kwa mfano ulioonyeshwa kule mlimani.”