Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Gospel: Unclassified scriptures relating to

87 mistari · 2 vipengele

Mistari kuhusu Unclassified scriptures relating to

Chuja kwa kitabu
  1. Kuna mto ambao vijito vyake vinaufurahisha mji wa Mungu, mahali patakatifu ambako Aliye Juu Sana anaishi.

  2. Mungu yuko katikati yake, hautaanguka, Mungu atausaidia asubuhi na mapema.

  3. Yesu akajibu, “Rudini mkamwambie Yohana yale mnayosikia na kuyaona:

  4. Vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa habari njema.

  5. Amebarikiwa mtu yule asiyechukizwa na mimi.”

  6. Yesu akawajia na kusema, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.

  7. Kwa sababu hii, enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu,

  8. nanyi wafundisheni kuyashika mambo yote niliyowaamuru ninyi. Hakika mimi niko pamoja nanyi siku zote, hadi mwisho wa nyakati.”

  9. Baada ya Yohana kukamatwa na kutiwa gerezani, Yesu aliingia Galilaya akaanza kuhubiri habari njema ya Mungu,

  10. akisema, “Wakati umewadia, Ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuiamini Habari Njema.”

  11. Zekaria, baba yake, akajazwa na Roho Mtakatifu, naye akatoa unabii, akisema:

  12. “Ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli, kwa kuwa amewajilia watu wake na kuwakomboa.

  13. Naye ametusimamishia pembe ya wokovu katika nyumba ya Daudi mtumishi wake,

  14. kama alivyonena kwa vinywa vya manabii wake watakatifu tangu zamani,

  15. kwamba atatuokoa kutoka kwa adui zetu, na kutoka mikononi mwao wote watuchukiao:

  16. ili kuonyesha rehema kwa baba zetu na kukumbuka Agano lake takatifu,

  17. kiapo alichomwapia baba yetu Abrahamu:

  18. kutuokoa kutoka mikononi mwa adui zetu, tupate kumtumikia yeye pasipo hofu

  19. katika utakatifu na haki mbele zake, siku zetu zote.

  20. “Nawe mtoto wangu, utaitwa nabii wa Aliye Juu Sana; kwa kuwa utamtangulia Bwana na kuandaa njia kwa ajili yake,

  21. kuwajulisha watu wake juu ya wokovu utakaopatikana kwa kusamehewa dhambi zao,

  22. kwa ajili ya wingi wa rehema za Mungu wetu, nuru itokayo juu itatuzukia

  23. ili kuwaangazia wale waishio gizani na katika uvuli wa mauti, kuiongoza miguu yetu katika njia ya amani.”

  24. Lakini malaika akawaambia: “Msiogope. Kwa maana tazama nawaletea habari njema za furaha itakayokuwa kwa watu wote.

  25. Leo katika mji wa Daudi kwa ajili yenu amezaliwa Mwokozi, ndiye Kristo Bwana.