Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Egyptians

71 mistari · 18 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Kizazi cha tatu cha watoto watakaozaliwa nao wanaweza kuingia katika kusanyiko la Bwana.

  2. siku aliyoonyesha ishara zake za ajabu huko Misri, maajabu yake huko Soani.

  3. Aligeuza mito yao kuwa damu, hawakuweza kunywa maji kutoka vijito vyao.

  4. Aliwapelekea makundi ya mainzi yakawala, na vyura wakawaharibu.

  5. Aliruhusu tunutu kuharibu mimea yao, mazao yao kwa nzige.

  6. Aliharibu mizabibu yao kwa mvua ya mawe na mikuyu yao kwa mvua iliyochangamana na theluji.

  7. Aliwaachia mifugo yao mvua ya mawe, akayapiga makundi ya wanyama wao kwa radi.

  8. Aliwafungulia hasira yake kali, ghadhabu yake, hasira na uadui, na kundi la malaika wa kuharibu.

  9. Aliitengenezea njia hasira yake, hakuwaepusha na kifo, bali aliwaachia tauni.

  10. Aliwapiga wazaliwa wote wa kwanza wa Misri, matunda ya kwanza ya ujana katika mahema ya Hamu.

  11. Jeshi la Farao lilikuwa limetoka Misri, nao Wakaldayo waliokuwa wameuzunguka Yerusalemu kwa majeshi waliposikia taarifa kuhusu jeshi hilo walijiondoa Yerusalemu.

  12. Ndipo neno la Bwana likamjia nabii Yeremia kusema:

  13. “Hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa Israeli: Mwambie mfalme wa Yuda aliyekutuma uniulize mimi, ‘Jeshi la Farao lililotoka kuja kukusaidia litarudi katika nchi yake yenyewe, yaani Misri.

  14. Kisha Wakaldayo watarudi na kushambulia mji huu, watauteka na kuuchoma moto.’

  15. “Hili ndilo Bwana asemalo: Msijidanganye wenyewe mkifikiri, ‘Hakika Wakaldayo watatuacha na kwenda zao.’ Hakika hawatawaacha!

  16. Hata kama mngelishinda jeshi lote la Wakaldayo linalowashambulia ninyi, na wakawa ni watu waliojeruhiwa tu waliobaki kwenye mahema yao, wangetoka na kuuchoma mji huu moto.”

  17. Baada ya jeshi la Wakaldayo kujiondoa kutoka Yerusalemu kwa sababu ya jeshi la Farao,

  18. Nitaifanya nchi ya Misri ukiwa, miongoni mwa nchi zilizo ukiwa, nayo miji yake itabaki ukiwa miaka arobaini miongoni mwa miji iliyo magofu. Nami nitawatawanya Wamisri miongoni mwa mataifa na kuwafukuza huku na huko katika nchi nyingine.

  19. “ ‘Lakini hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mwishoni mwa hiyo miaka arobaini, nitawakusanya Wamisri kutoka mataifa walikotawanywa.

  20. Nitawarudisha hao Wamisri kutoka kwenye kutekwa kwao na kuwaweka katika Pathrosi, nchi ya baba zao. Huko watakuwa na ufalme usiokuwa na nguvu.

  21. Utakuwa ufalme dhaifu kuliko zote na kamwe Misri haitajikweza tena juu ya mataifa mengine. Nitaufanya ufalme wake dhaifu sana kiasi kwamba kamwe hautatawala tena juu ya mataifa mengine.