Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Children: The gift of God

11 mistari · 102 vipengele

Mistari kuhusu The gift of God

  1. Lea akapata mimba akazaa mwana. Akamwita Reubeni, kwa maana alisema, “Ni kwa sababu Bwana ameona huzuni yangu. Hakika mume wangu sasa atanipenda.”

  2. Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana, akasema, “Kwa sababu Bwana alisikia kwamba sipendwi, amenipa tena huyu mwana.” Kwa hiyo akamwita Simeoni.

  3. Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana, akasema, “Sasa afadhali mume wangu ataambatana na mimi, kwa sababu nimemzalia wana watatu.” Kwa hiyo akamwita Lawi.

  4. Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana, akasema, “Wakati huu nitamsifu Bwana.” Kwa hiyo akamwita Yuda. Kisha akaacha kuzaa watoto.

  5. Mungu akamsikiliza Lea, naye akapata mimba akamzalia Yakobo mwana wa tano.

  6. Ndipo Lea akasema, “Mungu amenizawadia kwa kumpa mume wangu mtumishi wangu wa kike.” Kwa hiyo akamwita Isakari.

  7. Lea akapata mimba tena akamzalia Yakobo mwana wa sita.

  8. Ndipo Lea aliposema, “Mungu amenizawadia kwa zawadi ya thamani sana. Wakati huu mume wangu ataniheshimu kwa sababu nimemzalia wana sita.” Kwa hiyo akamwita Zabuloni.

  9. Ndipo Mungu akamkumbuka Raheli, akasikia maombi yake na akafungua tumbo lake.

  10. Akapata mimba na akamzaa mwana na kusema, “Mungu ameniondolea aibu yangu.”

  11. Akamwita Yosefu na kusema, “Bwana na anipe mwana mwingine.”