Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Chastity: General references

44 mistari · 21 vipengele

Mistari kuhusu General references

Chuja kwa kitabu
  1. Kwa maana hekima itaingia moyoni mwako, nayo maarifa yataifurahisha nafsi yako.

  2. Busara itakuhifadhi na ufahamu utakulinda.

  3. Itakuokoa pia kutokana na mwanamke kahaba, kutokana na mke aliyepotoka mwenye maneno ya kushawishi kutenda ubaya,

  4. aliyemwacha mwenzi wa ujana wake na kupuuza agano alilofanya mbele ya Mungu.

  5. Kwa maana nyumba yake huelekea kwenye kifo na mapito yake kwenye roho za waliokufa.

  6. Hakuna yeyote aendaye kwake akarudi, au kufikia mapito ya uzima.

  7. Hivyo utatembea katika njia za watu wema na kushikamana na mapito ya wenye haki.

  8. Kwa maana wanyofu wataishi katika nchi, nao wasio na lawama watabakia ndani yake.

  9. Bali waovu watakatiliwa mbali kutoka nchi, nao wasio waaminifu watangʼolewa kutoka humo.

  10. Kunywa maji kutoka kwenye kisima chako mwenyewe, maji yanayotiririka kutoka kwenye kisima chako mwenyewe.

  11. Je, chemchemi zako zifurike katika barabara za mji na vijito vyako vya maji viwanjani?

  12. Na viwe vyako mwenyewe, kamwe visishirikishwe wageni.

  13. Chemchemi yako na ibarikiwe na umfurahie mke wa ujana wako.

  14. Kulungu jike apendaye, kulungu mzuri: matiti yake na yakutosheleze siku zote, nawe utekwe daima na upendo wake.

  15. Kwa nini mwanangu, utekwe na mwanamke kahaba? Kwa nini ukumbatie kifua cha mke wa mwanaume mwingine?

  16. Kwa maana njia za mtu ni wazi kabisa mbele za Bwana, naye huyapima mapito yake yote.

  17. yakikulinda na mwanamke aliyepotoka, kutokana na maneno laini ya mwanamke aliyepotoka.

  18. Moyo wako usitamani uzuri wake wala macho yake yasikuteke,

  19. Mwanangu, shika maneno yangu na kuzihifadhi amri zangu ndani yako.

  20. Shika amri zangu nawe utaishi; linda mafundisho yangu kama mboni ya jicho lako.

  21. Yafunge katika vidole vyako; yaandike katika kibao cha moyo wako.

  22. Mwambie hekima, “Wewe ni dada yangu,” uite ufahamu jamaa yako;

  23. watakuepusha na mwanamke mzinzi, kutokana na mwanamke mpotovu na maneno yake ya kubembeleza.

  24. “Chakula ni cha tumbo, na tumbo ni la chakula”: lakini Mungu ataviangamiza vyote viwili. Mwili haukuumbwa kwa ajili ya zinaa bali kwa ajili ya Bwana na Bwana kwa ajili ya mwili.

  25. Naye Mungu aliyemfufua Bwana kutoka kwa wafu atatufufua sisi pia kwa uweza wake.