- English
- King James KJV
- Complete Jewish CJB
- World English WEBM
- Berean Standard BSB
- American Standard ASV
- Geneva GNV
- Young's Literal YLT
- Douay-Rheims DRC
- International
- Shqip ALB
- العربية SVD
- বাংলা BN-IRV
- မြန်မာ Judson
- 简体文 CUV-S
- 繁體中文 CUV-T
- Čeština BKR
- Nederlands STVE
- Français LSG
- Deutsch SCH
- Ελληνικά Vamvas
- ગુજરાતી GU-IRV
- Hausa HCB
- עברית Hebrew
- हिन्दी HCV
- Magyar KAROLI
- Bahasa Indonesia INDO-TB
- Italiano Diodati
- 日本語 Kougo
- 한국어 Korean
- മലയാളം MAL
- मराठी MRCV
- Norsk DNB
- فارسی OPV
- Polski BG
- Português Almeida
- Română Cornilescu
- Русский Synodal
- Español RVG
- Kiswahili Neno
- Svenska SV1917
- Tagalog TAG-ADB
- தமிழ் TCV
- తెలుగు TSA
- ภาษาไทย THAI-KJV
- Українська Ohienko
- Tiếng Việt CADMAN
- Yorùbá YCB
circa 1446–1406 BC
The Wilderness Years
Forty years of wandering in the desert test Israel's faith and prepare a new generation to enter the promised land.
Mistari ya kipindi hiki
- Kumbukumbu 27:20takriban 1451 KK
“Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mke wa baba yake, kwa maana anadharau malazi ya baba yake.”
- Kumbukumbu 27:21takriban 1451 KK
“Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mnyama yeyote.”
- Kumbukumbu 27:22takriban 1451 KK
“Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na dada yake, binti wa baba yake au binti wa mama yake.”
- Kumbukumbu 27:23takriban 1451 KK
“Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mama mkwe wake.”
- Kumbukumbu 27:24takriban 1451 KK
“Alaaniwe mtu amuuaye jirani yake kwa siri.”
- Kumbukumbu 27:25takriban 1451 KK
“Alaaniwe mtu apokeaye rushwa ili kumuua mtu asiye na hatia.”
- Kumbukumbu 27:26takriban 1451 KK
“Alaaniwe mtu yule ambaye hatashikilia maneno ya sheria hii kwa kuyatekeleza.”
- Kumbukumbu 28:1takriban 1451 KK
Kama ukimtii Bwana Mungu wako kwa bidii na kufuata amri zake zote ninazokupa leo kwa bidii, Bwana Mungu wako atakuweka juu ya mataifa yote katika dunia.
- Kumbukumbu 28:2takriban 1451 KK
Baraka hizi zote zitakuja juu yako na kukupata, kama ukimtii Bwana Mungu wako:
- Kumbukumbu 28:3takriban 1451 KK
Utabarikiwa mjini na utabarikiwa mashambani.
- Kumbukumbu 28:4takriban 1451 KK
Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na mazao ya nchi yako na wanyama wako wachanga wa kufugwa, yaani ndama wa makundi yako ya ngʼombe, na wana-kondoo wa makundi yako.
- Kumbukumbu 28:5takriban 1451 KK
Kapu lako na vyombo vyako vya kukandia vitabarikiwa.
- Kumbukumbu 28:6takriban 1451 KK
Utabarikiwa uingiapo na utabarikiwa utokapo.
- Kumbukumbu 28:7takriban 1451 KK
Bwana atasababisha adui wainukao dhidi yako kushindwa mbele yako. Watakujia kwa njia moja lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba.
- Kumbukumbu 28:8takriban 1451 KK
Bwana ataagiza baraka juu ya ghala zako na juu ya kila kitu utakachogusa kwa mkono wako. Bwana Mungu wako atakubariki katika nchi anayokupa.
- Kumbukumbu 28:9takriban 1451 KK
Bwana atakufanya kuwa taifa lake takatifu, kama alivyokuahidi kwa kiapo, kama ukishika maagizo ya Bwana Mungu wako na kwenda katika njia zake.
- Kumbukumbu 28:10takriban 1451 KK
Kisha mataifa yote ya dunia wataona kuwa unaitwa kwa jina la Bwana, nao watakuogopa.
- Kumbukumbu 28:11takriban 1451 KK
Bwana atakupa kustawi kwa wingi, katika tunda la uzao wa tumbo lako, katika wanyama wachanga wa mifugo yako na katika mazao ya ardhi yako, katika nchi aliyowaapia baba zako kuwapa.
- Kumbukumbu 28:12takriban 1451 KK
Bwana atafungua mbingu, ghala zake za baraka, kukupa mvua kwa majira yake na kubariki kazi zako zote za mikono yako. Utakopesha mataifa mengi lakini hutakopa kwa yeyote.
- Kumbukumbu 28:13takriban 1451 KK
Bwana atakufanya kichwa, wala si mkia. Kama utazingatia maagizo ya Bwana Mungu wako ninayokupa siku hii ya leo na kuyafuata kwa bidii, daima utakuwa juu, kamwe hutakuwa chini.
- Kumbukumbu 28:14takriban 1451 KK
Usihalifu amri zangu zozote ninazokupa leo, kwa kwenda kuume au kushoto, kwa kufuata miungu mingine na kuitumikia.
- Kumbukumbu 28:15takriban 1451 KK
Hata hivyo, kama hutamtii Bwana Mungu wako na kuzishika kwa bidii amri zake zote na maagizo ninayokupa leo, laana hizi zote zitakuja juu yako na kukupata:
- Kumbukumbu 28:16takriban 1451 KK
Utalaaniwa mjini na utalaaniwa mashambani.
- Kumbukumbu 28:17takriban 1451 KK
Kapu lako na chombo chako cha kukandia kitalaaniwa.
- Kumbukumbu 28:18takriban 1451 KK
Uzao wa tumbo lako utalaaniwa, mazao ya ardhi yako, ndama wa makundi yako ya ngʼombe na wana-kondoo wa makundi yako.