- English
- King James KJV
- Complete Jewish CJB
- World English WEBM
- Berean Standard BSB
- American Standard ASV
- Geneva GNV
- Young's Literal YLT
- Douay-Rheims DRC
- International
- Shqip ALB
- العربية SVD
- বাংলা BN-IRV
- မြန်မာ Judson
- 简体文 CUV-S
- 繁體中文 CUV-T
- Čeština BKR
- Nederlands STVE
- Français LSG
- Deutsch SCH
- Ελληνικά Vamvas
- ગુજરાતી GU-IRV
- Hausa HCB
- עברית Hebrew
- हिन्दी HCV
- Magyar KAROLI
- Bahasa Indonesia INDO-TB
- Italiano Diodati
- 日本語 Kougo
- 한국어 Korean
- മലയാളം MAL
- मराठी MRCV
- Norsk DNB
- فارسی OPV
- Polski BG
- Português Almeida
- Română Cornilescu
- Русский Synodal
- Español RVG
- Kiswahili Neno
- Svenska SV1917
- Tagalog TAG-ADB
- தமிழ் TCV
- తెలుగు TSA
- ภาษาไทย THAI-KJV
- Українська Ohienko
- Tiếng Việt CADMAN
- Yorùbá YCB
circa 1446–1406 BC
The Wilderness Years
Forty years of wandering in the desert test Israel's faith and prepare a new generation to enter the promised land.
Mistari ya kipindi hiki
- Kumbukumbu 13:8takriban 1451 KK
usikubali wala usimsikilize. Usimhurumie! Usimwache wala usimkinge.
- Kumbukumbu 13:9takriban 1451 KK
Hakika ni lazima auawe. Ni lazima mkono wako uwe wa kwanza katika kumuua kisha mikono ya watu wengine wote.
- Kumbukumbu 13:10takriban 1451 KK
Mpigeni kwa mawe mpaka afe, kwa sababu alijaribu kuwageuza mtoke kwa Bwana Mungu wenu ambaye aliwatoa Misri, kutoka nchi ya utumwa.
- Kumbukumbu 13:11takriban 1451 KK
Kisha Israeli wote watasikia na kuogopa, wala hakuna mmoja miongoni mwenu atakayefanya uovu tena.
- Kumbukumbu 13:12takriban 1451 KK
Kama mkisikia ikisemwa kwamba moja ya miji ambayo Bwana Mungu wenu anawapa mkae ndani yake
- Kumbukumbu 13:13takriban 1451 KK
kuna wanaume waovu wameinuka miongoni mwenu na wamewapotosha watu wa mji, wakisema, “Twendeni tukaabudu miungu mingine” (miungu ambayo hamkuifahamu),
- Kumbukumbu 13:14takriban 1451 KK
ndipo itakubidi kuuliza, kupima na kuchunguza kwa makini. Kama ni kweli, tena ikihakikishwa kwamba jambo hili lichukizalo limefanyika miongoni mwenu,
- Kumbukumbu 13:15takriban 1451 KK
kwa hakika ni lazima mwaue kwa upanga wale wote wanaoishi katika mji ule. Uharibuni kabisa, pamoja na watu wake na mifugo yake.
- Kumbukumbu 13:16takriban 1451 KK
Kusanyeni nyara zote za mji katika uwanja wa wazi na kuuchoma mji kabisa pamoja na nyara zake zote kama sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana Mungu wenu. Utabaki kuwa magofu milele na hautajengwa tena.
- Kumbukumbu 13:17takriban 1451 KK
Hakuna kimoja kati ya vitu vilivyolaaniwa kitakachokutwa mikononi mwenu, ili Bwana ageuze hasira yake kali. Atawahurumia na kuwa na rehema kwenu pia kuongeza idadi yenu, kama alivyowaahidi baba zenu,
- Kumbukumbu 13:18takriban 1451 KK
kwa sababu mnamtii Bwana Mungu wenu, mkizishika amri zake zote zile ninazowapa leo na kufanya lile lililo jema machoni pake.
- Kumbukumbu 14:1takriban 1451 KK
Ninyi ni watoto wa Bwana Mungu wenu. Msijichanje ama kujinyoa upara kwenye paji la uso kwa ajili ya aliyekufa,
- Kumbukumbu 14:2takriban 1451 KK
kwa maana ninyi ni taifa takatifu kwa Bwana Mungu wenu. Bwana amewachagua ninyi kuwa taifa la kipekee kutoka mataifa yote juu ya uso wa dunia, mwe tunu yake.
- Kumbukumbu 14:3takriban 1451 KK
Msile kitu chochote ambacho ni machukizo.
- Kumbukumbu 14:4takriban 1451 KK
Hawa ndio wanyama mtakaokula: ngʼombe, kondoo, mbuzi,
- Kumbukumbu 14:5takriban 1451 KK
kulungu, paa, kongoni, paa mweupe, mbuzi-mwitu, pofu na kondoo wa mlimani.
- Kumbukumbu 14:6takriban 1451 KK
Mnaweza kumla mnyama yeyote mwenye kwato zilizogawanyika mara mbili, pia yule anayecheua.
- Kumbukumbu 14:7takriban 1451 KK
Hata hivyo, miongoni mwa wale wanaocheua au wale walio na kwato zilizogawanyika kamwe msile ngamia, sungura na pelele. Iwapo wanacheua, lakini hawana kwato zilizogawanyika; ni najisi kwenu kwa taratibu za kiibada.
- Kumbukumbu 14:8takriban 1451 KK
Nguruwe pia ni najisi; ingawa ana kwato zilizogawanyika, hacheui. Msile nyama yake wala kugusa mzoga wake.
- Kumbukumbu 14:9takriban 1451 KK
Katika viumbe hai vyote viishivyo kwenye maji, mnaweza kula yeyote aliye na mapezi na magamba.
- Kumbukumbu 14:10takriban 1451 KK
Lakini chochote kisicho na mapezi na magamba msile; kwenu ni najisi.
- Kumbukumbu 14:11takriban 1451 KK
Mnaweza kula ndege yeyote aliye safi.
- Kumbukumbu 14:12takriban 1451 KK
Lakini wafuatao msiwale: tai, furukombe, kipungu,
- Kumbukumbu 14:13takriban 1451 KK
kengewa mwekundu, kengewa mweusi, mwewe wa aina yoyote,
- Kumbukumbu 14:14takriban 1451 KK
kunguru wa aina yoyote,