Rukia maudhui

circa 1446–1406 BC

The Wilderness Years

Forty years of wandering in the desert test Israel's faith and prepare a new generation to enter the promised land.

2,247 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Kumbukumbu 11:22takriban 1491 KK

    Kama mkishika kwa makini maagizo haya yote ninayowapa kuyafuata, ya kumpenda Bwana Mungu wenu, kuenenda katika njia zake zote na kushikamana naye kwa uthabiti,

  2. Kumbukumbu 11:23takriban 1491 KK

    ndipo Bwana atawafukuza mataifa haya yote mbele yako, nawe utawafukuza mataifa yaliyo makubwa na yenye nguvu kukuliko wewe.

  3. Kumbukumbu 11:24takriban 1491 KK

    Kila mahali mtakapoweka mguu wenu patakuwa penu: Nchi yenu itaenea kutoka jangwa la Lebanoni, na kutoka mto wa Frati hadi bahari ya magharibi

  4. Kumbukumbu 11:25takriban 1491 KK

    Hapatakuwa na mtu atakayeweza kusimama dhidi yenu. Bwana Mungu wenu, kama alivyoahidi, ataweka juu ya nchi yote utisho na hofu kwa ajili yenu popote mwendako.

  5. Kumbukumbu 11:26takriban 1491 KK

    Tazama, leo ninaweka mbele yenu baraka na laana:

  6. Kumbukumbu 11:27takriban 1491 KK

    baraka kama mtatii maagizo ya Bwana Mungu wenu, ambayo ninawapa leo;

  7. Kumbukumbu 11:28takriban 1491 KK

    laana kama hamtatii maagizo ya Bwana Mungu wenu na kuacha njia ambayo ninawaamuru leo kwa kufuata miungu mingine, ambayo hamkuijua.

  8. Kumbukumbu 11:29takriban 1491 KK

    Wakati Bwana Mungu wenu atakapokuwa amewaleta katika nchi mnayoiingia kuimiliki, mtatangaza baraka kutoka Mlima Gerizimu, na kutangaza laana kutoka Mlima Ebali.

  9. Kumbukumbu 11:30takriban 1491 KK

    Kama mnavyofahamu, milima hii ipo ngʼambo ya Yordani, magharibi ya barabara, kuelekea machweo ya jua, karibu na miti mikubwa ya More, katika nchi ya wale Wakanaani wanaoishi Araba, jirani na Gilgali.

  10. Kumbukumbu 11:31takriban 1491 KK

    Karibu mvuke ngʼambo ya Yordani kuingia na kuimiliki nchi ambayo Bwana Mungu wenu anawapa. Wakati mtakapokuwa mmeichukua na mnaishi humo,

  11. Kumbukumbu 11:32takriban 1491 KK

    hakikisheni kwamba mnatii amri na sheria zote ninazoziweka mbele yenu leo.

  12. Kumbukumbu 12:1takriban 1451 KK

    Hizi ndizo amri na sheria ambazo ni lazima mwe waangalifu kuzifuata katika nchi ambayo Bwana, Mungu wa baba zenu, amewapa kumiliki, kwa muda wote mtakaoishi katika nchi.

  13. Kumbukumbu 12:2takriban 1451 KK

    Haribuni kabisa kila mahali pao pa kuabudia kwenye milima mirefu, vilima na chini ya kila mti mkubwa ambamo mataifa haya mnayokwenda kuchukua ardhi yao huabudia miungu yao.

  14. Kumbukumbu 12:3takriban 1451 KK

    Bomoeni madhabahu zao, vunjeni yale mawe wanayoabudu, chomeni moto nguzo zao za Ashera; katilieni mbali sanamu za miungu yao na mfute majina yao mahali hapo.

  15. Kumbukumbu 12:4takriban 1451 KK

    Kamwe msimwabudu Bwana Mungu wenu kama wanavyoabudu wao.

  16. Kumbukumbu 12:5takriban 1451 KK

    Bali mtatafuta mahali Bwana Mungu wenu atakapopachagua katika makabila yenu yote ili aliweke jina lake huko kuwa makao yake. Mahali hapo ndipo iwapasapo kwenda;

  17. Kumbukumbu 12:6takriban 1451 KK

    hapo ndipo mtakapoleta sadaka zenu za kuteketezwa na dhabihu, zaka zenu na changizo zenu, kile ulichoweka nadhiri kutoa, sadaka zenu za hiari na malimbuko ya makundi yenu ya ngʼombe pamoja na mbuzi na kondoo.

  18. Kumbukumbu 12:7takriban 1451 KK

    Hapo, katika uwepo wa Bwana Mungu wenu, ninyi pamoja na jamaa zenu, mtakula na kufurahia kila kitu ambacho mmegusa kwa mikono yenu, kwa sababu Bwana Mungu wenu amewabariki.

  19. Kumbukumbu 12:8takriban 1451 KK

    Msifanye kama tunavyofanya hapa leo, kila mtu anavyopenda mwenyewe,

  20. Kumbukumbu 12:9takriban 1451 KK

    kwa kuwa bado hamjafikia mahali pa mapumziko na urithi ambao Bwana Mungu wenu anawapa.

  21. Kumbukumbu 12:10takriban 1451 KK

    Lakini mtavuka Yordani na kuishi katika nchi Bwana Mungu wenu anayowapa kama urithi, naye atawapa pumziko kutokana na adui zenu wote wanaowazunguka ili ninyi mpate kuishi kwa salama.

  22. Kumbukumbu 12:11takriban 1451 KK

    Kisha kuhusu mahali Bwana Mungu wenu atakapopachagua kuwa mahali pa makao ya Jina lake, hapo ndipo inapowapasa kuleta kila kitu ninachowaamuru: sadaka zenu za kuteketezwa na dhabihu, zaka zenu na changizo, pamoja na vitu vyote vyenye thamani ambavyo mmeweka nadhiri kumtolea Bwana.

  23. Kumbukumbu 12:12takriban 1451 KK

    Hapo furahini mbele za Bwana Mungu wenu, ninyi, wana wenu na binti zenu, watumishi wenu wa kiume na wa kike, pamoja na Walawi kutoka miji yenu ambao hawana mgawo wala urithi wao wenyewe.

  24. Kumbukumbu 12:13takriban 1451 KK

    Kuweni waangalifu, msitoe dhabihu zenu za kuteketezwa mahali popote mnapopapenda.

  25. Kumbukumbu 12:14takriban 1451 KK

    Mtazitoa tu mahali pale ambapo Bwana atachagua katika mojawapo ya makabila yenu, nanyi hapo zingatieni kila jambo ninalowaamuru.