Rukia maudhui

circa 6 BC – AD 30

The Life of Jesus

The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.

3,779 mistari · 4 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Luka 12:11takriban 33 BK

    “Watakapowapeleka katika masinagogi, na mbele ya watawala na wenye mamlaka, msiwe na wasiwasi kuhusu namna mtakavyojitetea au mtakavyosema.

  2. Luka 12:12takriban 33 BK

    Kwa maana Roho Mtakatifu atawafundisha wakati huo huo mnachopaswa kusema.”

  3. Luka 12:13takriban 33 BK

    Mtu mmoja katika umati wa watu akamwambia Yesu, “Mwalimu, mwambie ndugu yangu tugawane naye urithi wetu.”

  4. Luka 12:14takriban 33 BK

    Lakini Yesu akamwambia, “Rafiki, ni nani aliyeniweka mimi kuwa hakimu wenu au msuluhishi juu yenu?”

  5. Luka 12:15takriban 33 BK

    Ndipo Yesu akawaambia, “Jihadharini! Jilindeni na aina zote za choyo. Kwa maana maisha ya mtu hayatokani na wingi wa mali alizo nazo.”

  6. Luka 12:16takriban 33 BK

    Kisha akawaambia mfano huu: “Shamba la mtu mmoja tajiri lilizaa sana.

  7. Luka 12:17takriban 33 BK

    Akawaza moyoni mwake, ‘Nifanye nini? Sina mahali pa kuhifadhi mavuno yangu.’

  8. Luka 12:18takriban 33 BK

    “Ndipo huyo tajiri akasema, ‘Nitafanya hivi: Nitabomoa ghala zangu za nafaka na kujenga nyingine kubwa zaidi na huko nitayahifadhi mavuno yangu yote na vitu vyangu.

  9. Luka 12:19takriban 33 BK

    Nami nitaiambia nafsi yangu, “Nafsi, unavyo vitu vingi vizuri ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi. Pumzika; kula, unywe, ufurahi.” ’

  10. Luka 12:20takriban 33 BK

    “Lakini Mungu akamwambia, ‘Mpumbavu wewe! Usiku huu uhai wako unatakiwa. Sasa hivyo vitu ulivyojiwekea akiba vitakuwa vya nani?’

  11. Luka 12:21takriban 33 BK

    “Hivyo ndivyo ilivyo kwa wale wanaojiwekea mali lakini hawajitajirishi kwa Mungu.”

  12. Luka 12:22takriban 33 BK

    Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake: “Kwa hiyo nawaambia, msisumbukie maisha yenu kwamba mtakula nini; au msumbukie miili yenu kwamba mtavaa nini.

  13. Luka 12:23takriban 33 BK

    Maisha ni zaidi ya chakula, na mwili ni zaidi ya mavazi.

  14. Luka 12:24takriban 33 BK

    Fikirini ndege! Wao hawapandi wala hawavuni, hawana ghala wala popote pa kuhifadhi nafaka; lakini Mungu huwalisha. Ninyi ni wa thamani zaidi kuliko ndege!

  15. Luka 12:25takriban 33 BK

    Ni nani miongoni mwenu ambaye kwa kujitaabisha kwake anaweza kujiongezea hata saa moja zaidi katika maisha yake?

  16. Luka 12:26takriban 33 BK

    Kama hamwezi kufanya jambo dogo kama hilo, kwa nini basi kuyasumbukia hayo mengine?

  17. Luka 12:27takriban 33 BK

    “Angalieni maua jinsi yameavyo: Hayafanyi kazi wala hayafumi. Lakini nawaambia, hata Solomoni katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo ya hayo maua.

  18. Luka 12:28takriban 33 BK

    Basi ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya shambani, ambayo leo yapo, na kesho yanatupwa motoni, si atawavika ninyi vizuri zaidi, enyi wa imani haba!

  19. Luka 12:29takriban 33 BK

    Wala msisumbuke mioyoni mwenu mtakula nini au mtakunywa nini. Msiwe na wasiwasi juu ya haya.

  20. Luka 12:30takriban 33 BK

    Watu wa mataifa ya duniani husumbuka sana kuhusu vitu hivi vyote, lakini Baba yenu anafahamu kuwa mnahitaji haya yote.

  21. Luka 12:31takriban 33 BK

    Bali utafuteni Ufalme wa Mungu, na haya yote atawapa pia.

  22. Luka 12:32takriban 33 BK

    “Msiogope enyi kundi dogo, kwa maana Baba yenu ameona vyema kuwapa ninyi Ufalme.

  23. Luka 12:33takriban 33 BK

    Uzeni mali zenu mkawape maskini. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, mkajiwekee hazina mbinguni isiyokwisha, mahali ambapo mwizi hakaribii wala nondo haharibu.

  24. Luka 12:34takriban 33 BK

    Kwa sababu mahali hazina yako ilipo, hapo ndipo moyo wako utakapokuwa pia.

  25. Luka 12:35takriban 33 BK

    “Kuweni tayari mkiwa mmevikwa kwa ajili ya huduma na taa zenu zikiwa zinawaka,