Rukia maudhui

circa 6 BC – AD 30

The Life of Jesus

The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.

3,779 mistari · 4 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Marko 7:32takriban 32 BK

    Huko, watu wakamletea Yesu mtu mmoja kiziwi, ambaye pia alikuwa na kigugumizi, wakamwomba aweke mkono wake juu ya huyo mtu na amponye.

  2. Marko 7:33takriban 32 BK

    Baadaye Yesu akampeleka yule kiziwi kando mbali na watu, Yesu akatia vidole vyake masikioni mwa yule mtu. Kisha akatema mate na kuugusa ulimi wa yule mtu.

  3. Marko 7:34takriban 32 BK

    Ndipo Yesu akatazama mbinguni, akavuta hewa ndani kwa nguvu akamwambia, “Efatha!” (yaani, “Funguka!”)

  4. Marko 7:35takriban 32 BK

    Mara masikio yake yakafunguka na ulimi wake ukaachiliwa, akaanza kuongea sawasawa.

  5. Marko 7:36takriban 32 BK

    Yesu akawaamuru wasimwambie mtu yeyote habari hizi. Lakini kadiri alivyowazuia, ndivyo walivyozidi kutangaza kwa bidii.

  6. Marko 7:37takriban 32 BK

    Walistaajabu mno. Wakasema, “Amefanya mambo yote vizuri mno! Amewawezesha viziwi wasikie na bubu waseme!”

  7. Marko 8:1takriban 32 BK

    Katika siku hizo, umati mkubwa wa watu ulikusanyika tena. Kwa kuwa walikuwa hawana chakula, Yesu akawaita wanafunzi wake akawaambia,

  8. Marko 8:2takriban 32 BK

    “Ninauhurumia huu umati wa watu, kwa sababu sasa wamekuwa nami kwa muda wa siku tatu na hawana chakula.

  9. Marko 8:3takriban 32 BK

    Nikiwaaga waende nyumbani bila kula, watazimia njiani kwa sababu baadhi yao wametoka mbali.”

  10. Marko 8:4takriban 32 BK

    Wanafunzi wake wakamjibu, “Lakini hapa nyikani tutapata wapi mikate ya kutosha kuwalisha?”

  11. Marko 8:5takriban 32 BK

    Yesu akawauliza, “Mna mikate mingapi?” Wakajibu, “Tuna mikate saba.”

  12. Marko 8:6takriban 32 BK

    Akawaambia watu waketi chini. Akiisha kuichukua mikate saba na kushukuru, akaimega na kuwapa wanafunzi wake ili wawagawie watu. Wanafunzi wake wakafanya hivyo.

  13. Marko 8:7takriban 32 BK

    Walikuwa pia na visamaki vichache, Yesu akavibariki, akawaamuru wanafunzi wake wawagawie watu.

  14. Marko 8:8takriban 32 BK

    Wale watu walikula na kutosheka. Baadaye wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu saba.

  15. Marko 8:9takriban 32 BK

    Watu waliokula walikuwa wapata 4,000. Akiisha kuwaaga,

  16. Marko 8:10takriban 32 BK

    aliingia kwenye mashua pamoja na wanafunzi wake, akaenda sehemu za Dalmanutha.

  17. Marko 8:11takriban 32 BK

    Mafarisayo wakaja, wakaanza kumhoji Yesu. Ili kumtega, wakamwomba awaonyeshe ishara kutoka mbinguni.

  18. Marko 8:12takriban 32 BK

    Akahuzunika moyoni, akawaambia, “Kwa nini kizazi hiki kinataka ishara? Amin nawaambieni, hakitapewa ishara yoyote.”

  19. Marko 8:13takriban 32 BK

    Kisha akawaacha, akarudi kwenye mashua, akavuka hadi ngʼambo.

  20. Marko 8:14takriban 32 BK

    Wanafunzi walikuwa wamesahau kuchukua mikate ya kutosha. Walikuwa na mkate mmoja tu kwenye mashua.

  21. Marko 8:15takriban 32 BK

    Yesu akawaonya: “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo na ya Herode.”

  22. Marko 8:16takriban 32 BK

    Wakajadiliana wao kwa wao, na kusema, “Anasema hivi kwa sababu hatukuleta mikate.”

  23. Marko 8:17takriban 32 BK

    Yesu, akifahamu majadiliano yao, akawauliza: “Mbona mnajadiliana kuhusu kutokuwa na mikate? Je, bado hamtambui wala hamwelewi? Je, mbona mioyo yenu ni migumu kiasi hicho?

  24. Marko 8:18takriban 32 BK

    Je, mna macho lakini mnashindwa kuona, na mna masikio lakini mnashindwa kusikia? Je, hamkumbuki?

  25. Marko 8:19takriban 32 BK

    Nilipoimega ile mikate mitano kuwalisha watu 5,000, mlikusanya vikapu vingapi vilivyojaa vya masazo?” Wakamjibu, “Kumi na viwili.”