circa 6 BC – AD 30
The Life of Jesus
The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.
Mistari ya kipindi hiki
- Marko 6:38takriban 28 BK
Akawauliza, “Kuna mikate mingapi? Nendeni mkaangalie.” Walipokwisha kujua wakarudi, wakamwambia, “Kuna mikate mitano na samaki wawili.”
- Marko 6:39takriban 28 BK
Kisha Yesu akawaamuru wawaketishe watu makundi makundi kwenye majani,
- Marko 6:40takriban 28 BK
nao wakaketi kwenye makundi ya watu mia mia na wengine hamsini hamsini.
- Marko 6:41takriban 28 BK
Yesu akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akainua macho yake akatazama mbinguni, akavibariki na kuimega ile mikate. Kisha akawapa wanafunzi wake ili wawagawie wale watu wote. Pia akawagawia wote wale samaki wawili.
- Marko 6:42takriban 28 BK
Watu wote wakala, wakashiba.
- Marko 6:43takriban 28 BK
Nao wanafunzi wake wakakusanya vipande vilivyosalia vya mikate na samaki, wakajaza vikapu kumi na viwili.
- Marko 6:44takriban 28 BK
Idadi ya wanaume waliokula walikuwa 5,000.
- Marko 6:45takriban 28 BK
Mara Yesu akawaambia wanafunzi wake waingie kwenye mashua watangulie kwenda Bethsaida, wakati yeye alikuwa akiwaaga wale makutano.
- Marko 6:46takriban 28 BK
Baada ya kuwaaga wale watu, akaenda mlimani kuomba.
- Marko 6:47takriban 28 BK
Ilipofika jioni, ile mashua ilikuwa imefika katikati ya bahari, na Yesu alikuwa peke yake katika nchi kavu.
- Marko 6:48takriban 28 BK
Akawaona wanafunzi wake wanahangaika na kupiga makasia kwa nguvu, kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho. Wakati wa zamu ya nne ya usiku, Yesu akawaendea wanafunzi wake, akiwa anatembea juu ya maji. Alikuwa karibu kuwapita,
- Marko 6:49takriban 28 BK
lakini walipomwona akitembea juu ya maji, wakadhani ni mzimu. Wakapiga yowe,
- Marko 6:50takriban 28 BK
kwa sababu wote walipomwona waliogopa. Mara Yesu akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo! Ni mimi. Msiogope!”
- Marko 6:51takriban 28 BK
Akapanda ndani ya mashua nao, na ule upepo ukakoma! Wakashangaa kabisa,
- Marko 6:52takriban 28 BK
kwa kuwa walikuwa hawajaelewa kuhusu ile mikate. Mioyo yao ilikuwa migumu.
- Marko 6:53takriban 28 BK
Walipokwisha kuvuka, wakafika nchi ya Genesareti, wakatia nanga.
- Marko 6:54takriban 28 BK
Mara waliposhuka kutoka mashua yao, watu wakamtambua Yesu.
- Marko 6:55takriban 28 BK
Wakaenda katika vijiji vyote upesi, wakawabeba wagonjwa kwenye mikeka ili kuwapeleka mahali popote waliposikia kuwa Yesu yupo.
- Marko 6:56takriban 28 BK
Kila mahali Yesu alipokwenda, iwe vijijini, mijini au mashambani, watu waliwaweka wagonjwa wao masokoni. Wakamwomba awaruhusu hao wagonjwa waguse japo upindo wa vazi lake. Nao wote waliomgusa waliponywa.
- Marko 7:1takriban 32 BK
Mafarisayo na baadhi ya walimu wa sheria waliokuwa wametoka Yerusalemu wakakusanyika mbele ya Yesu.
- Marko 7:2takriban 32 BK
Wakawaona baadhi ya wanafunzi wake wakila chakula kwa mikono iliyo najisi, yaani, bila kunawa kama ilivyotakiwa na sheria ya dini ya Wayahudi.
- Marko 7:3takriban 32 BK
(Kwa kuwa Mafarisayo na Wayahudi wote hawali chakula pasipo kunawa kwa kufuata desturi za wazee wao.
- Marko 7:4takriban 32 BK
Wanapotoka sokoni hawawezi kula pasipo kunawa. Pia kuna desturi nyingine nyingi wanazofuata kama vile jinsi ya kuosha vikombe, vyungu na vyombo vya shaba.)
- Marko 7:5takriban 32 BK
Kwa hiyo wale Mafarisayo na walimu wa sheria wakamuuliza Yesu, “Mbona wanafunzi wako hawafuati desturi za wazee, na badala yake wanakula kwa mikono najisi?”
- Marko 7:6takriban 32 BK
Yesu akawajibu, “Nabii Isaya alisema ukweli alipotabiri juu yenu, ninyi wanafiki. Kama ilivyoandikwa: “ ‘Watu hawa huniheshimu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali nami.