Rukia maudhui

circa 6 BC – AD 30

The Life of Jesus

The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.

3,779 mistari · 4 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Marko 7:7takriban 32 BK

    Huniabudu bure, nayo mafundisho yao ni maagizo ya wanadamu tu.’

  2. Marko 7:8takriban 32 BK

    Ninyi mmeziacha amri za Mungu na kushika desturi za watu.”

  3. Marko 7:9takriban 32 BK

    Naye akawaambia, “Ninyi mnayo njia nzuri ya kukataa amri za Mungu ili mpate kuyashika mapokeo yenu!

  4. Marko 7:10takriban 32 BK

    Kwa mfano, Mose alisema, ‘Waheshimu baba yako na mama yako,’ na, ‘Yeyote amtukanaye baba yake au mama yake, na auawe.’

  5. Marko 7:11takriban 32 BK

    Lakini ninyi mwafundisha kwamba mtu akimwambia baba yake au mama yake, ‘Kile ambacho ningeweza kukusaidia ni Korbani’ (yaani kimewekwa wakfu kwa Mungu),

  6. Marko 7:12takriban 32 BK

    basi hawajibiki tena kumsaidia baba yake au mama yake.

  7. Marko 7:13takriban 32 BK

    Kwa njia hiyo ninyi mnabatilisha neno la Mungu kwa mapokeo yenu mliyojiwekea. Nanyi mnafanya mambo mengi ya aina hiyo.”

  8. Marko 7:14takriban 32 BK

    Yesu akaita tena ule umati wa watu, akawaambia, “Nisikilizeni, kila mmoja wenu na mwelewe jambo hili.

  9. Marko 7:15takriban 32 BK

    Hakuna kitu kinachomwingia mtu kimtiacho unajisi, lakini kile kimtokacho ndicho kimtiacho unajisi. [

  10. Marko 7:16takriban 32 BK

    Kama mtu yeyote ana masikio ya kusikia na asikie.]”

  11. Marko 7:17takriban 32 BK

    Akiisha kuuacha ule umati wa watu na kuingia ndani, wanafunzi wake wakamuuliza maana ya mfano ule.

  12. Marko 7:18takriban 32 BK

    Akawajibu, “Je, hata nanyi hamwelewi? Je, hamfahamu kwamba kitu kimwingiacho mtu hakimtii unajisi?

  13. Marko 7:19takriban 32 BK

    Mtu akila kitu hakiingii moyoni mwake bali tumboni, na baadaye hutolewa nje ya mwili wake.” (Kwa kusema hivi, Yesu alivihalalisha vyakula vyote kuwa ni “safi.”)

  14. Marko 7:20takriban 32 BK

    Akaendelea kusema, “Kile kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi.

  15. Marko 7:21takriban 32 BK

    Kwa maana kutoka ndani ya moyo wa mtu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wizi, uuaji, uzinzi,

  16. Marko 7:22takriban 32 BK

    tamaa mbaya, uovu, udanganyifu, ufisadi, wivu, matukano, kiburi na upumbavu.

  17. Marko 7:23takriban 32 BK

    Maovu haya yote hutoka ndani ya mtu, nayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi.”

  18. Marko 7:24takriban 32 BK

    Ndipo Yesu akaondoka hapo akaenda sehemu za Tiro. Akaingia katika nyumba moja, naye hakutaka mtu yeyote ajue kwamba yuko humo. Lakini hakuweza kujificha.

  19. Marko 7:25takriban 32 BK

    Mara mwanamke mmoja, ambaye binti yake mdogo alikuwa na pepo mchafu, akaja na kumpigia magoti miguuni pake.

  20. Marko 7:26takriban 32 BK

    Basi huyo mwanamke alikuwa Myunani, aliyezaliwa Foinike ya Siria. Akamsihi Yesu amtoe binti yake huyo pepo mchafu.

  21. Marko 7:27takriban 32 BK

    Yesu akamwambia, “Waache watoto washibe kwanza, kwa maana si vyema kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.”

  22. Marko 7:28takriban 32 BK

    Lakini yule mwanamke akamjibu, “Bwana, hata mbwa walio chini ya meza hula makombo ya chakula cha watoto.”

  23. Marko 7:29takriban 32 BK

    Ndipo Yesu akamjibu, “Kwa sababu ya jibu lako, nenda zako nyumbani; yule pepo mchafu amemtoka binti yako.”

  24. Marko 7:30takriban 32 BK

    Akaenda zake nyumbani akamkuta binti yake amelala kitandani, yule pepo mchafu akiwa amemtoka.

  25. Marko 7:31takriban 32 BK

    Kisha Yesu akaondoka sehemu za Tiro, akapita katikati ya Sidoni, hadi Bahari ya Galilaya na kuingia eneo la Dekapoli.