Rukia maudhui

circa 1380–1050 BC

The Judges & Ruth

Israel cycles through rebellion, oppression, and rescue under charismatic leaders—culminating in Ruth's faithful love story.

703 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Waamuzi 9:31takriban 1233 KK

    Akatuma ujumbe uende kwa Abimeleki kwa siri na kusema, “Gaali mwana wa Ebedi na ndugu zake wamekuja Shekemu, na wanauchochea mji huu kinyume chako.

  2. Waamuzi 9:32takriban 1233 KK

    Sasa, basi, usiku huu wewe uondoke na watu wako ili mje kuwavizia mashambani.

  3. Waamuzi 9:33takriban 1233 KK

    Kisha asubuhi wakati wa kuchomoza jua, amka mapema na ujipange dhidi ya huo mji. Wakati yeye na jeshi lililo pamoja naye watakapotoka kukabiliana nanyi, mwaweza kuwatendea kwa kadiri mnavyoweza.”

  4. Waamuzi 9:34takriban 1233 KK

    Kwa hiyo Abimeleki pamoja na jeshi lake lote wakaondoka usiku na kujificha karibu na Shekemu wakiwa vikosi vinne.

  5. Waamuzi 9:35takriban 1233 KK

    Basi Gaali mwana wa Ebedi alikuwa ametoka nje akawa amesimama katika ingilio la mji wakati ule ule ambao Abimeleki na watu wake walipokuwa wanatoka sehemu zao za maficho.

  6. Waamuzi 9:36takriban 1233 KK

    Gaali alipowaona, akamwambia Zebuli, “Tazama, watu wanashuka kutoka kwenye vilele vya milima!” Zebuli akajibu, “Wewe unaona vivuli vya milima kana kwamba ni watu.”

  7. Waamuzi 9:37takriban 1233 KK

    Lakini Gaali akasema tena, “Tazama, watu wanashuka kutoka katikati ya nchi na kikosi kimoja kinakuja kutoka Tabur-Ezeri na kikosi kingine kutoka upande wa Elon-Meonenimu.”

  8. Waamuzi 9:38takriban 1233 KK

    Ndipo Zebuli akamwambia, “Kuko wapi kujivuna kwako sasa, wewe uliyesema, ‘Huyo Abimeleki ni nani hata tumtumikie?’ Hawa si wale watu uliowadharau? Toka nje sasa ukapigane nao!”

  9. Waamuzi 9:39takriban 1233 KK

    Basi Gaali akatoka akawaongoza watu wa Shekemu kupigana na Abimeleki.

  10. Waamuzi 9:40takriban 1233 KK

    Abimeleki akamfukuza, watu wengi wakajeruhiwa katika kukimbia huko, njia nzima hadi kwenye ingilio la lango.

  11. Waamuzi 9:41takriban 1233 KK

    Abimeleki akakaa Aruma, naye Zebuli akawafukuza Gaali na ndugu zake watoke Shekemu.

  12. Waamuzi 9:42takriban 1233 KK

    Kesho yake watu wa Shekemu wakatoka wakaenda mashambani, Abimeleki akaambiwa juu ya jambo hili.

  13. Waamuzi 9:43takriban 1233 KK

    Hivyo akawachukua watu wake, akawagawanya katika vikosi vitatu na kuwaweka waviziao huko mashambani. Alipowaona watu wanatoka kwenda nje ya mji, akainuka dhidi yao na kuwashambulia.

  14. Waamuzi 9:44takriban 1233 KK

    Abimeleki pamoja na vile vikosi wakaharakisha kwenda mbele kwenye nafasi, mahali pa ingilio la lango la mji. Vile vikosi viwili vikawawahi wale waliokuwa mashambani na kuwaua.

  15. Waamuzi 9:45takriban 1233 KK

    Siku hiyo nzima Abimeleki akazidisha mashambulizi yake dhidi ya mji hadi akawa ameuteka na kuwaua watu wa huo mji. Kisha akauangamiza mji na kusambaza chumvi juu yake.

  16. Waamuzi 9:46takriban 1233 KK

    Kwa kusikia jambo hili watu wote katika mnara wa Shekemu, wakaingia kwenye ngome ya hekalu la El-Berithi.

  17. Waamuzi 9:47takriban 1233 KK

    Abimeleki aliposikia kuwa wamekusanyika huko,

  18. Waamuzi 9:48takriban 1233 KK

    yeye na watu wake wote wakakwea kwenye Mlima Salmoni. Abimeleki akachukua shoka, akakata baadhi ya matawi, ambayo aliyachukua mabegani. Akawaagiza wale watu waliokuwa pamoja naye kuwa, “Fanyeni kile mlichoona mimi nikifanya!”

  19. Waamuzi 9:49takriban 1233 KK

    Basi watu wote wakakata matawi na kumfuata Abimeleki. Wakayakusanya hayo matawi juu ya ngome na kuitia moto ili kuwachoma wale watu wote waliokuwa ndani yake. Hivyo watu wote katika mnara wa Shekemu, karibia watu 1,000 waume kwa wake, pia wakafa.

  20. Waamuzi 9:50takriban 1233 KK

    Baadaye Abimeleki akaenda Thebesi na kuuzingira kwa jeshi na kuuteka.

  21. Waamuzi 9:51takriban 1233 KK

    Hata hivyo, ndani ya huo mji kulikuwa na mnara imara, ambako watu wote wa mji wanaume na wanawake, watu wote wa mji, walikimbilia ndani yake. Wakajifungia ndani yake na kupanda juu ya paa la mnara.

  22. Waamuzi 9:52takriban 1233 KK

    Abimeleki akaja kwenye ule mnara na kuushambulia, lakini alipokaribia kwenye ingilio la mnara ili kuuchoma kwa moto,

  23. Waamuzi 9:53takriban 1233 KK

    mwanamke mmoja akaangusha sehemu ya juu ya jiwe la kusagia juu ya kichwa cha Abimeleki, likapasua fuvu la kichwa chake.

  24. Waamuzi 9:54takriban 1233 KK

    Akamwita kwa haraka kijana yule aliyechukua silaha zake, na kumwambia, “Chukua upanga wako na uniue, watu wasije wakasema kwamba, ‘Mwanamke amemuua.’ ” Basi yule kijana akamchoma upanga, naye akafa.

  25. Waamuzi 9:55takriban 1233 KK

    Waisraeli walipoona kuwa Abimeleki amekufa, kila mtu akaenda nyumbani kwake.