Rukia maudhui

circa 800–400 BC

The Hebrew Prophets

God speaks through Isaiah, Jeremiah, and the minor prophets—calling Israel to repentance and foretelling the coming Messiah.

3,706 mistari · 14 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Isaya 62:1takriban 698 KK

    Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza, kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, mpaka haki yake itakapoangaza kama mapambazuko, wokovu wake kama mwanga wa moto.

  2. Isaya 62:2takriban 698 KK

    Mataifa wataona haki yako, nao wafalme wote wataona utukufu wako; wewe utaitwa kwa jina jipya lile ambalo kinywa cha Bwana kitatamka.

  3. Isaya 62:3takriban 698 KK

    Utakuwa taji ya fahari mkononi mwa Bwana, taji ya kifalme mkononi mwa Mungu wako.

  4. Isaya 62:4takriban 698 KK

    Hawatakuita tena Aliyeachwa, wala nchi yako kuiita Ukiwa. Bali utaitwa Hefsiba, nayo nchi yako itaitwa Beula, kwa maana Bwana atakufurahia, nayo nchi yako itaolewa.

  5. Isaya 62:5takriban 698 KK

    Kama vile kijana aoavyo mwanamwali, ndivyo wanao watakavyokuoa wewe; kama bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi wake, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe.

  6. Isaya 62:6takriban 698 KK

    Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, ee Yerusalemu, hawatanyamaza mchana wala usiku. Ninyi wenye kumwita Bwana, msitulie,

  7. Isaya 62:7takriban 698 KK

    msimwache apumzike hadi atakapoufanya imara Yerusalemu na kuufanya uwe sifa ya dunia.

  8. Isaya 62:8takriban 698 KK

    Bwana ameapa kwa mkono wake wa kuume na kwa mkono wake wenye nguvu: “Kamwe sitawapa tena adui zenu nafaka zenu kama chakula chao; kamwe wageni hawatakunywa tena divai mpya ambayo mmeitaabikia,

  9. Isaya 62:9takriban 698 KK

    lakini wale waivunao nafaka wataila na kumsifu Bwana, nao wale wakusanyao zabibu watainywa divai yake katika nyua za patakatifu pangu.”

  10. Isaya 62:10takriban 698 KK

    Piteni, piteni katika malango! Tengenezeni njia kwa ajili ya watu. Jengeni, jengeni njia kuu! Ondoeni mawe. Inueni bendera kwa ajili ya mataifa.

  11. Isaya 62:11takriban 698 KK

    Bwana ametoa tangazo mpaka miisho ya dunia: “Mwambie Binti Sayuni, ‘Tazama, mwokozi wako anakuja! Tazama ujira wake uko pamoja naye, na malipo yake yanafuatana naye!’ ”

  12. Isaya 62:12takriban 698 KK

    Wataitwa Watu Watakatifu, Waliokombolewa na Bwana; nawe utaitwa Aliyetafutwa, Mji Usioachwa Tena.

  13. Isaya 63:1takriban 698 KK

    Ni nani huyu anayekuja kutoka Edomu, kutoka Bosra, mwenye mavazi yaliyotiwa madoa mekundu? Ni nani huyu, aliyevikwa joho la kifahari, anayetembea kwa ukuu wa nguvu zake? “Mimi ndimi, nisemaye katika haki, mwenye nguvu wa kuokoa.”

  14. Isaya 63:2takriban 698 KK

    Kwa nini mavazi yako ni mekundu, kama ya yule akanyagaye shinikizo la zabibu?

  15. Isaya 63:3takriban 698 KK

    “Nimekanyaga shinikizo la zabibu peke yangu; kutoka mataifa hakuna mtu aliyekuwa pamoja nami. Nimewaponda kwa miguu katika hasira yangu na kuwakanyaga chini katika ghadhabu yangu; damu yao ilitia matone kwenye mavazi yangu, na kutia madoa nguo zangu zote.

  16. Isaya 63:4takriban 698 KK

    Kwa kuwa siku ya kisasi ilikuwa moyoni mwangu, mwaka wa ukombozi wangu umefika.

  17. Isaya 63:5takriban 698 KK

    Nilitazama, lakini hakuwepo yeyote wa kunisaidia, nilishangaa kwa kuwa hakuwepo yeyote aliyetoa msaada; hivyo mkono wangu wenyewe ndio ulionifanyia wokovu, na ghadhabu yangu mwenyewe ndiyo iliyonitegemeza.

  18. Isaya 63:6takriban 698 KK

    Nilikanyaga mataifa kwa miguu katika hasira yangu, katika ghadhabu yangu niliwalewesha, na kumwaga damu yao juu ya ardhi.”

  19. Isaya 63:7takriban 698 KK

    Nitasimulia juu ya wema wa Bwana, kwa matendo ambayo apaswa kusifiwa, sawasawa na yote ambayo Bwana ametenda kwa ajili yetu: naam, mambo mengi mema aliyoyatenda kwa ajili ya nyumba ya Israeli, sawasawa na huruma zake na wema wake mwingi.

  20. Isaya 63:8takriban 698 KK

    Alisema, “Hakika wao ni watu wangu, wana ambao hawatanidanganya”; hivyo akawa Mwokozi wao.

  21. Isaya 63:9takriban 698 KK

    Katika taabu zao zote naye alitaabika, na malaika wa uso wake akawaokoa. Katika upendo wake na rehema zake aliwakomboa, akawainua na kuwachukua siku zote zilizopita.

  22. Isaya 63:10takriban 698 KK

    Lakini waliasi, na kumhuzunisha Roho Mtakatifu wake. Hivyo aligeuka na kuwa adui yao, na yeye mwenyewe akapigana dhidi yao.

  23. Isaya 63:11takriban 698 KK

    Ndipo watu wake wakazikumbuka siku zilizopita, siku za Mose na watu wake: yuko wapi yeye aliyewaleta kupitia katikati ya bahari, pamoja na wachungaji wa kundi lake? Yuko wapi yule aliyeweka Roho wake Mtakatifu katikati yao,

  24. Isaya 63:12takriban 698 KK

    aliyetuma mkono wake uliotukuka wenye nguvu kuwa katika mkono wa kuume wa Mose, aliyegawa maji ya bahari mbele yao, ili kujipatia jina milele,

  25. Isaya 63:13takriban 698 KK

    aliyewaongoza kupitia kwenye vilindi? Kama farasi katika nchi iliyo wazi, wao hawakujikwaa,