Rukia maudhui

circa AD 30–62

The Early Church

Pentecost ignites a movement; Peter, Paul, and countless others carry the gospel from Jerusalem to the ends of the earth.

1,007 mistari · 1 kitabu kimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

  1. Matendo 20:23takriban 60 BK

    Ila ninachojua tu ni kwamba Roho Mtakatifu amenionya kuwa vifungo na mateso vinaningoja.

  2. Matendo 20:24takriban 60 BK

    Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa ya thamani kwangu, kama kuyamaliza mashindano na kukamilisha ile kazi Bwana Yesu aliyonipa, yaani, kazi ya kuishuhudia Injili ya neema ya Mungu.

  3. Matendo 20:25takriban 60 BK

    “Nami sasa najua ya kuwa hakuna hata mmoja miongoni mwenu ambaye nimemhubiria Ufalme wa Mungu katika kwenda kwangu huku na huko, atakayeniona uso tena.

  4. Matendo 20:26takriban 60 BK

    Kwa hiyo nawatangazia leo, sina hatia ya damu ya mtu awaye yote.

  5. Matendo 20:27takriban 60 BK

    Kwa kuwa sikusita kuwatangazia mapenzi yote ya Mungu.

  6. Matendo 20:28takriban 60 BK

    Jilindeni nafsi zenu na mlilinde lile kundi lote ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi wake. Lichungeni kanisa lake Mungu alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.

  7. Matendo 20:29takriban 60 BK

    Najua kwamba baada yangu kuondoka, mbwa mwitu wakali watakuja katikati yenu ambao hawatalihurumia kundi.

  8. Matendo 20:30takriban 60 BK

    Hata kutoka miongoni mwenu watainuka watu na kuupotosha ukweli ili wawavute wanafunzi wawafuate.

  9. Matendo 20:31takriban 60 BK

    Hivyo jilindeni! Kumbukeni kwamba kwa miaka mitatu sikuacha kamwe kuwaonya kila mmoja kwa machozi usiku na mchana.

  10. Matendo 20:32takriban 60 BK

    “Sasa nawakabidhi kwa Mungu na kwa neno la neema yake, linaloweza kuwajenga na kuwapa ninyi urithi miongoni mwa wote ambao wametakaswa.

  11. Matendo 20:33takriban 60 BK

    Sikutamani fedha wala dhahabu wala vazi la mtu yeyote.

  12. Matendo 20:34takriban 60 BK

    Ninyi wenyewe mnajua kwamba mikono yangu hii imetumika kwa mahitaji yangu na ya wale waliokuwa pamoja nami.

  13. Matendo 20:35takriban 60 BK

    Katika kila jambo nimewaonyesha kwamba kwa njia hii ya kufanya kazi kwa bidii imetupasa kuwasaidia wadhaifu, mkikumbuka maneno ya Bwana Yesu mwenyewe jinsi alivyosema, ‘Ni heri kutoa kuliko kupokea.’ ”

  14. Matendo 20:36takriban 60 BK

    Paulo alipomaliza kusema haya akapiga magoti pamoja nao wote akaomba.

  15. Matendo 20:37takriban 60 BK

    Wote wakalia, wakamkumbatia Paulo na kumbusu,

  16. Matendo 20:38takriban 60 BK

    Kilichowahuzunisha zaidi ni kwa sababu ya yale maneno aliyosema kwamba kamwe hawatauona uso wake tena. Wakaenda naye mpaka kwenye meli.

  17. Matendo 21:1takriban 60 BK

    Tulipokwisha kujitenga nao, tukaanza safari kwa njia ya bahari moja kwa moja mpaka Kosi. Siku ya pili yake tukafika Rodo na kutoka huko tukaenda Patara.

  18. Matendo 21:2takriban 60 BK

    Hapo tukapata meli iliyokuwa inavuka kwenda Foinike tukapanda tukasafiri nayo.

  19. Matendo 21:3takriban 60 BK

    Tulipokiona kisiwa cha Kipro, tukakizunguka tukakiacha upande wetu wa kushoto, tukasafiri mpaka Shamu, tukatia nanga katika bandari ya Tiro ambapo meli yetu ilikuwa ipakue shehena yake.

  20. Matendo 21:4takriban 60 BK

    Baada ya kuwatafuta wanafunzi wa huko, tukakaa nao kwa siku saba. Wale wanafunzi wakiongozwa na Roho wakamwambia Paulo asiende Yerusalemu.

  21. Matendo 21:5takriban 60 BK

    Lakini muda wetu ulipokwisha, tukaondoka tukaendelea na safari yetu. Wale wanafunzi pamoja na wake zao na watoto wakatusindikiza hadi nje ya mji. Wote tukapiga magoti pale pwani tukaomba.

  22. Matendo 21:6takriban 60 BK

    Baada ya kuagana, tukapanda melini, nao wakarudi majumbani mwao.

  23. Matendo 21:7takriban 60 BK

    Tukaendelea na safari yetu toka Tiro tukafika Tolemai, tukawasalimu ndugu wa huko, tukakaa nao kwa siku moja.

  24. Matendo 21:8takriban 60 BK

    Siku iliyofuata tukaondoka, tukafika Kaisaria. Huko tukaenda nyumbani kwa mwinjilisti mmoja jina lake Filipo, aliyekuwa mmoja wa wale Saba, tukakaa kwake.

  25. Matendo 21:9takriban 60 BK

    Filipo alikuwa na binti wanne mabikira waliokuwa wanatoa unabii.