Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Adui zake nitawavika aibu, bali taji kichwani pake itangʼaa sana.”

  2. Ni kama vile umande wa Hermoni unavyoanguka juu ya Mlima Sayuni. Kwa maana huko ndiko Bwana alikoamuru baraka yake, naam, hata uzima milele.

  3. Wimbo wa kwenda juu. Msifuni Bwana, ninyi nyote watumishi wa Bwana, ninyi mnaotumika usiku ndani ya nyumba ya Bwana.

  4. Inueni mikono yenu katika pale patakatifu na kumsifu Bwana.

  5. Naye Bwana, Muumba wa mbingu na dunia, awabariki kutoka Sayuni.

  6. Msifuni Bwana. Lisifuni jina la Bwana, msifuni, enyi watumishi wa Bwana,

  7. ninyi ambao mnatumika ndani ya nyumba ya Bwana, katika nyua za nyumba ya Mungu wetu.

  8. Msifuni Bwana, kwa kuwa Bwana ni mwema, liimbieni sifa jina lake, kwa maana hilo lapendeza.

  9. Kwa maana Bwana amemchagua Yakobo kuwa wake mwenyewe, Israeli kuwa mali yake ya thamani.

  10. Ninajua ya kuwa Bwana ni mkuu, kwamba Bwana wetu ni mkuu kuliko miungu yote.

  11. Bwana hufanya lolote apendalo, mbinguni na duniani, katika bahari na vilindi vyake vyote.

  12. Hufanya mawingu kupanda kutoka miisho ya dunia; hupeleka umeme wa radi pamoja na mvua na huleta upepo kutoka ghala zake.

  13. akatoa nchi yao kuwa urithi, urithi kwa watu wake Israeli.

  14. Ee Bwana, jina lako ladumu milele, kumbukumbu za fahari zako, Ee Bwana, kwa vizazi vyote.

  15. Maana Bwana atawathibitisha watu wake, na kuwahurumia watumishi wake.

  16. Ee nyumba ya Israeli, msifuni Bwana; ee nyumba ya Aroni, msifuni Bwana;

  17. ee nyumba ya Lawi, msifuni Bwana; ninyi mnaomcha, msifuni Bwana.

  18. Msifuni Bwana kutoka Sayuni, msifuni yeye aishiye Yerusalemu. Msifuni Bwana.

  19. Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema. Fadhili zake zadumu milele.

  20. Mshukuruni Mungu wa miungu. Fadhili zake zadumu milele.

  21. Mshukuruni Bwana wa mabwana: Fadhili zake zadumu milele.

  22. Kwake yeye pekee atendaye maajabu makuu, Fadhili zake zadumu milele.

  23. Ambaye kwa ufahamu wake aliziumba mbingu, Fadhili zake zadumu milele.

  24. Ambaye aliitandaza dunia juu ya maji, Fadhili zake zadumu milele.

  25. Ambaye aliumba mianga mikubwa, Fadhili zake zadumu milele.