Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Wale wapitao karibu na wasiseme, “Baraka ya Bwana iwe juu yako; tunakubariki katika jina la Bwana.”

  2. Wimbo wa kwenda juu. Kutoka vilindini ninakulilia, Ee Bwana.

  3. Ee Bwana, sikia sauti yangu. Masikio yako na yawe masikivu kwa kilio changu unihurumie.

  4. Kama wewe, Ee Bwana, ungeweka kumbukumbu ya dhambi, Ee Bwana, ni nani angeliweza kusimama?

  5. Lakini kwako kuna msamaha, kwa hiyo wewe unaogopwa.

  6. Namngojea Bwana, nafsi yangu inangojea, katika neno lake naweka tumaini langu.

  7. Nafsi yangu inamngojea Bwana kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi, naam, kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi.

  8. Ee Israeli, mtumaini Bwana, maana kwa Bwana kuna upendo usiokoma, na kwake kuna ukombozi kamili.

  9. Yeye mwenyewe ataikomboa Israeli kutoka dhambi zao zote.

  10. Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. Moyo wangu hauna kiburi, Ee Bwana, macho yangu hayajivuni; sijishughulishi na mambo makuu kunizidi wala mambo ya ajabu mno kwangu.

  11. Ee Israeli, mtumaini Bwana tangu sasa na hata milele.

  12. Wimbo wa kwenda juu. Ee Bwana, mkumbuke Daudi na taabu zote alizozistahimili.

  13. Aliapa kiapo kwa Bwana na akaweka nadhiri kwa Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo:

  14. mpaka nitakapompatia Bwana mahali, makao kwa ajili ya Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo.”

  15. “Twendeni kwenye makao yake, na tuabudu kwenye kiti cha kuwekea miguu yake;

  16. inuka, Ee Bwana, uje mahali pako pa kupumzikia, wewe na Sanduku la nguvu zako.

  17. Makuhani wako na wavikwe haki, watakatifu wako na waimbe kwa furaha.”

  18. Kwa ajili ya Daudi mtumishi wako, usimkatae mpakwa mafuta wako.

  19. Bwana alimwapia Daudi kiapo, kiapo cha uhakika ambacho hatakitangua: “Nitamweka mmoja wa wazao wako mwenyewe katika kiti chako cha enzi,

  20. kama wanao watashika Agano langu na sheria ninazowafundisha, ndipo wana wao watarithi kiti chako cha enzi milele na milele.”

  21. Kwa maana Bwana ameichagua Sayuni, amepaonea shauku pawe maskani yake:

  22. “Hapa ni mahali pangu pa kupumzika milele na milele; hapa ndipo nitakapoketi nikitawala, kwa sababu nimepaonea shauku:

  23. Nitambariki kwa kumpa mahitaji tele: nitashibisha maskini wake kwa chakula.

  24. Nitawavika makuhani wake wokovu, nao watakatifu wake watadumu wakiimba kwa furaha.

  25. “Hapa nitamchipushia Daudi pembe, na kuweka taa kwa ajili ya masiya wangu.