Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Wao na waimbe kuhusu njia za Bwana, kwa maana utukufu wa Bwana ni mkuu.

  2. Ingawa Bwana yuko juu, humwangalia mnyonge, bali mwenye kiburi yeye anamjua kutokea mbali.

  3. Nijapopita katikati ya shida, wewe unayahifadhi maisha yangu, unanyoosha mkono wako dhidi ya hasira ya adui zangu, kwa mkono wako wa kuume unaniokoa.

  4. Bwana atatimiza kusudi lake kwangu, Ee Bwana, upendo wako wadumu milele: usiziache kazi za mikono yako.

  5. Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Ee Bwana, umenichunguza na kunijua.

  6. Unajua ninapoketi na ninapoinuka; unatambua mawazo yangu tokea mbali.

  7. Kabla neno halijafika katika ulimi wangu, wewe walijua kikamilifu, Ee Bwana.

  8. Umenizunguka nyuma na mbele; umeweka mkono wako juu yangu.

  9. Niende wapi nijiepushe na Roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako?

  10. Kama nikienda juu mbinguni, wewe uko huko; nikifanya vilindi kuwa kitanda changu, wewe uko huko.

  11. hata huko mkono wako utaniongoza, mkono wako wa kuume utanishika kwa uthabiti.

  12. hata giza halitakuwa giza kwako, usiku utangʼaa kama mchana, kwa kuwa giza ni kama nuru kwako.

  13. Kwa maana wewe ndiwe uliyeumba utu wangu wa ndani; uliniunga pamoja tumboni mwa mama yangu.

  14. Ninakusifu kwa sababu nimeumbwa kwa namna ya ajabu na ya kutisha; kazi zako ni za ajabu, ninajua hayo kikamilifu.

  15. Umbile langu halikufichika kwako, nilipoumbwa mahali pa siri. Nilipoungwa pamoja kwa ustadi katika vilindi vya nchi,

  16. macho yako yaliniona kabla mwili wangu haujakamilika. Siku zangu zote ulizonipangia ziliandikwa katika kitabu chako kabla haijakuwepo hata moja.

  17. Tazama jinsi yalivyo ya thamani mawazo yako kwangu, Ee Mungu! Jinsi jumla yake ilivyo kubwa!

  18. Kama ningezihesabu, zingekuwa nyingi kuliko mchanga. Niamkapo, bado niko pamoja nawe.

  19. Laiti ungewachinja waovu, Ee Mungu! Ondokeni kwangu, ninyi wamwaga damu!

  20. Wanazungumza juu yako wakiwa na kusudi baya, adui zako wanatumia vibaya jina lako.

  21. Ee Bwana, je, nisiwachukie wanaokuchukia? Nisiwachukie sana wanaoinuka dhidi yako?

  22. Ee Mungu, nichunguze, uujue moyo wangu, nijaribu na ujue mawazo yangu.

  23. Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Ee Bwana, niokoe, kutoka kwa watu waovu; nilinde na watu wenye jeuri,

  24. Ee Bwana, niepushe na mikono ya waovu; nilinde na watu wenye jeuri wanaopanga kunikwaza miguu yangu.

  25. Ee Bwana, ninakuambia, “Wewe ni Mungu wangu.” Ee Bwana, usikie kilio changu na kunihurumia.