Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Ee Bwana, mwanadamu ni nini hata umjali, Binadamu ni nini hata umfikirie?

  2. Ee Bwana, pasua mbingu zako, ushuke, gusa milima ili itoe moshi.

  3. Peleka umeme uwatawanye adui, lenga mishale yako uwashinde.

  4. Nyoosha mkono wako kutoka juu, nikomboe na kuniokoa kutoka maji makuu, kutoka mikononi mwa wageni

  5. Ee Mungu, nitakuimbia wimbo mpya, kwa zeze yenye nyuzi kumi nitakuimbia,

  6. kwa Yule awapaye wafalme ushindi, ambaye humwokoa Daudi, mtumishi wake kutokana na upanga hatari.

  7. Heri watu ambao hili ni kweli; heri wale ambao Bwana ni Mungu wao.

  8. Wimbo wa Sifa. Wa Daudi. Nitakutukuza wewe, Mungu wangu Mfalme, nitalisifu jina lako milele na milele.

  9. Kila siku nitakusifu na kulitukuza jina lako milele na milele.

  10. Bwana ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana, ukuu wake haupimiki.

  11. Kizazi kimoja kitasifia kazi zako kwa kizazi kingine, watasimulia matendo yako makuu.

  12. Watasema juu ya utukufu wa fahari ya ukuu wako, nami nitatafakari juu ya kazi zako za ajabu.

  13. Watasimulia uwezo wa kazi zako za kutisha, nami nitatangaza matendo yako makuu.

  14. Wataadhimisha wema wako mwingi, na wataimba kwa shangwe juu ya haki yako.

  15. Bwana ni mwenye neema na mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira, bali ni mwingi wa upendo.

  16. Bwana ni mwema kwa wote, ana huruma kwa vyote alivyovifanya.

  17. Ee Bwana, vyote ulivyovifanya vitakusifu, watakatifu wako watakutukuza.

  18. Watasimulia utukufu wa ufalme wako na kusema juu ya ukuu wako,

  19. ili watu wote wajue matendo yako makuu na utukufu wa fahari ya ufalme wako.

  20. Ufalme wako ni ufalme wa milele, mamlaka yako hudumu vizazi vyote. Bwana ni mwaminifu kwa ahadi zake zote na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya.

  21. Bwana huwategemeza wote waangukao, na huwainua wote waliolemewa na mizigo yao.

  22. Macho yao wote yanakutazama wewe, nawe huwapa chakula chao wakati wake.

  23. Waufumbua mkono wako, watosheleza haja ya kila kitu kilicho hai.

  24. Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote, na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya.

  25. Bwana yu karibu na wote wamwitao, karibu na wote wamwitao kwa uaminifu.