God
Mistari inayomtaja God
Hajafanya hivyo kwa taifa lingine lolote, hawazijui sheria zake. Msifuni Bwana.
Msifuni Bwana. Msifuni Bwana kutoka mbinguni, msifuni juu vileleni.
Msifuni, enyi malaika wake wote, msifuni yeye, enyi jeshi lake lote la mbinguni.
Msifuni yeye, enyi jua na mwezi, msifuni yeye, enyi nyota zote zingʼaazo.
Msifuni yeye, enyi mbingu zilizo juu sana, na ninyi maji juu ya anga.
Vilisifu jina la Bwana kwa maana aliamuru navyo vikaumbwa.
Aliviweka mahali pake milele na milele, alitoa amri ambayo haibadiliki milele.
Mtukuzeni Bwana kutoka duniani, ninyi viumbe vikubwa vya baharini na vilindi vyote vya bahari,
umeme wa radi na mvua ya mawe, theluji na mawingu, pepo za dhoruba zinazofanya amri zake,
Wote na walisifu jina la Bwana, kwa maana jina lake pekee limetukuka, utukufu wake uko juu ya nchi na mbingu.
Amewainulia watu wake pembe, sifa ya watakatifu wake wote, ya Israeli, watu walio karibu na moyo wake. Msifuni Bwana.
Msifuni Bwana. Mwimbieni Bwana wimbo mpya, sifa zake katika kusanyiko la watakatifu.
Israeli na washangilie katika Muumba wao, watu wa Sayuni na wafurahi katika Mfalme wao.
Na walisifu jina lake kwa kucheza na wampigie muziki kwa matari na kinubi.
Kwa maana Bwana anapendezwa na watu wake, anawavika wanyenyekevu taji ya wokovu.
Sifa za Mungu na ziwe vinywani mwao na upanga ukatao kuwili mikononi mwao,
ili kuwafanyia hukumu iliyoandikwa dhidi yao. Huu ndio utukufu wa watakatifu wake wote. Msifuni Bwana.
Msifuni Bwana. Msifuni Mungu katika patakatifu pake, msifuni katika mbingu zake kuu.
Msifuni kwa matendo yake makuu, msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.
Msifuni kwa mvumo wa tarumbeta, msifuni kwa kinubi na zeze,
msifuni kwa matari na kucheza, msifuni kwa kinanda cha nyuzi na filimbi,
msifuni kwa matoazi yaliayo, msifuni kwa matoazi yavumayo sana.
Kila chenye pumzi na kimsifu Bwana. Msifuni Bwana!
Kumcha Bwana ndicho chanzo cha maarifa, lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu.
Kama mngekuwa mmeitikia karipio langu, ningekuwa nimemimina roho yangu kwenu na kuwafahamisha maneno yangu.