Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Huwatimizia wamchao matakwa yao, husikia kilio chao na kuwaokoa.

  2. Bwana huwalinda wote wampendao, bali waovu wote atawaangamiza.

  3. Kinywa changu kitazinena sifa za Bwana. Kila kiumbe na kilisifu jina lake takatifu milele na milele.

  4. Msifuni Bwana! Ee nafsi yangu, umsifu Bwana,

  5. Nitamsifu Bwana maisha yangu yote; nitamwimbia Mungu wangu sifa wakati wote niishipo.

  6. Heri yeye ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake, ambaye tumaini lake ni katika Bwana, Mungu wake,

  7. Naye huwapatia haki walioonewa na kuwapa wenye njaa chakula. Bwana huwaweka wafungwa huru,

  8. Bwana huwafumbua vipofu macho, Bwana huwainua waliolemewa na mizigo yao, Bwana huwapenda wenye haki.

  9. Bwana huwalinda wageni na kuwategemeza yatima na wajane, lakini hupinga njia za waovu.

  10. Bwana atamiliki milele, Mungu wako, ee Sayuni, kwa vizazi vyote. Msifuni Bwana.

  11. Msifuni Bwana. Tazama jinsi ilivyo vyema kumwimbia Mungu wetu sifa, jinsi inavyopendeza na kustahili kumsifu yeye!

  12. Bwana hujenga Yerusalemu, huwakusanya Israeli walio uhamishoni.

  13. Huzihesabu nyota na huipa kila moja jina lake.

  14. Bwana wetu ni mkuu na mwenye uwezo mwingi, ufahamu wake hauna kikomo.

  15. Bwana huwahifadhi wanyenyekevu lakini huwashusha waovu mpaka mavumbini.

  16. Mwimbieni Bwana kwa shukrani, mpigieni Mungu wetu kinubi.

  17. Furaha yake haipo katika nguvu za farasi, wala furaha yake kwenye miguu ya mwanadamu.

  18. Bwana hupendezwa na wale wamchao, wale wanaoweka tumaini lao katika upendo wake usiokoma.

  19. Mtukuze Bwana, ee Yerusalemu, msifu Mungu wako, ee Sayuni,

  20. kwa maana huimarisha makomeo ya malango yako na huwabariki watu wako walio ndani yako.

  21. Hutuma amri yake duniani, neno lake hukimbia kasi.

  22. Anatandaza theluji kama sufu na kutawanya umande kama majivu.

  23. Huvurumisha mvua yake ya mawe kama changarawe. Ni nani awezaye kustahimili ukali wa baridi yake?

  24. Hutuma neno lake na kuviyeyusha, huvumisha upepo wake, nayo maji hutiririka.

  25. Amemfunulia Yakobo neno lake, sheria zake na maagizo yake kwa Israeli.