Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu The, Are Compared To Wicked

58 mistari · 55 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Watu wa miji hiyo wameishiwa nguvu, wanavunjika mioyo na kuaibishwa. Wao ni kama mimea katika shamba, kama machipukizi mororo ya kijani, kama majani yachipuayo juu ya paa la nyumba, ambayo hukauka kabla ya kukua.

  2. Mpumbavu aweza kuwa mwenye hekima, endapo mtoto wa punda-mwitu atazaliwa mwanadamu.

  3. Kama ndoto hutoweka, wala hapatikani tena, amefukuziwa mbali kama maono ya usiku.

  4. Ni mara ngapi huwa kama majani makavu mbele ya upepo, kama makapi yachukuliwayo na dhoruba?

  5. Sivyo walivyo waovu! Wao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.

  6. Wamefanana na simba mwenye njaa awindaye, kama simba mkubwa anyemeleaye mafichoni.

  7. Wakati utakapojitokeza utawafanya kama tanuru ya moto. Katika ghadhabu yake Bwana atawameza, moto wake utawateketeza.

  8. Mafahali wengi wamenizunguka, mafahali wa Bashani wenye nguvu wamenizingira.

  9. kwa maana kama majani watanyauka mara, kama mimea ya kijani watakufa mara.

  10. Nimemwona mtu mwovu na mkatili akistawi kama mwerezi wa Lebanoni,

  11. Lakini mwanadamu, licha ya utajiri wake, hadumu; anafanana na mnyama aangamiaye.

  12. Sumu yao ni kama sumu ya nyoka, kama ile ya fira ambaye ameziba masikio yake,

  13. Kama vile moshi upeperushwavyo na upepo, vivyo hivyo uwapeperushe mbali, kama vile nta iyeyukavyo kwenye moto, vivyo hivyo waovu na waangamie mbele za Mungu.

  14. Ee Mungu wangu, wapeperushe kama mavumbi ya kisulisuli, kama makapi yapeperushwayo na upepo.

  15. ingawa waovu huchipua kama majani na wote watendao mabaya wanastawi, wataangamizwa milele.

  16. Wale wanaozitengeneza watafanana nazo, vivyo hivyo wale wote wanaozitumainia.

  17. Walinizunguka kama kundi la nyuki, lakini walikufa haraka kama miiba iteketeayo; kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.

  18. Waovu wa nchi unawatupa kama takataka, kwa hivyo nazipenda sheria zako.

  19. Tufani inapopita, waovu hutoweka, lakini wenye haki husimama imara milele.

  20. Kama mbwa ayarudiavyo matapiko yake, ndivyo mpumbavu arudiavyo upumbavu wake.

  21. Kama rangi ingʼaayo iliyopakwa kwenye vyombo vya udongo ndivyo ilivyo midomo laini pamoja na moyo mbaya.

  22. Mtakuwa kama mwaloni wenye majani yanayonyauka, kama bustani isiyokuwa na maji.

  23. Kwa hasira ya Bwana Mwenye Nguvu Zote nchi itachomwa kwa moto, nao watu watakuwa kuni za kuchochea moto. Hakuna mtu atakayemhurumia ndugu yake.

  24. Lakini wewe umetupwa nje ya kaburi lako kama tawi lililokataliwa, umefunikwa na waliouawa pamoja na wale waliochomwa kwa upanga, wale washukao mpaka kwenye mawe ya shimo. Kama mzoga uliokanyagwa chini ya nyayo,

  25. Ni Bwana Mwenyezi anisaidiaye mimi. Ni nani huyo atakayenihukumu? Wote watachakaa kama vazi, nondo watawala wawamalize.