Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Solomon: Divides his kingdom into subsistence departments; the daily subsistence rate for his court

19 mistari · 46 vipengele

Mistari kuhusu Divides his kingdom into subsistence departments; the daily subsistence rate for his court

  1. Pia Solomoni alikuwa na watawala kumi na wawili wa wilaya katika Israeli yote, walioleta mahitaji kwa mfalme na kwa watu wa nyumbani kwa mfalme. Kila mmoja alitoa chakula kwa mwezi mmoja katika mwaka.

  2. Majina yao ni haya: Ben-Huri: katika nchi ya vilima ya Efraimu;

  3. Ben-Dekeri: katika Makasi, Shaalbimu, Beth-Shemeshi na Elon-Bethhanani;

  4. Ben-Hesedi: katika Arubothi (Soko na nchi yote ya Heferi zilikuwa zake);

  5. Ben-Abinadabu: katika Nafoth-Dori (alimwoa Tafathi binti Solomoni);

  6. Baana mwana wa Ahiludi: katika Taanaki na Megido, na katika Beth-Shani yote karibu na Sarethani chini ya Yezreeli, kuanzia Beth-Shani hadi Abel-Mehola kupita hadi Yokmeamu;

  7. Ben-Geberi: katika Ramoth-Gileadi (makao ya Yairi mwana wa Manase katika Gileadi ilikuwa miji yake, pamoja na wilaya ya Argobu katika Bashani na miji yake mikubwa sitini yenye kuzungukwa na kuta zenye makomeo ya shaba);

  8. Ahinadabu mwana wa Ido: katika Mahanaimu;

  9. Ahimaasi: katika Naftali (alikuwa amemwoa Basemathi binti Solomoni);

  10. Baana mwana wa Hushai: katika Asheri na katika Bealothi;

  11. Yehoshafati mwana wa Parua: katika Isakari;

  12. Shimei mwana wa Ela: katika Benyamini;

  13. Geberi mwana wa Uri: katika Gileadi (nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori na nchi ya Ogu mfalme wa Bashani). Naye alikuwa ndiye mtawala pekee katika eneo hilo.

  14. Watu wa Yuda na Israeli walikuwa wengi kama mchanga wa pwani; walikula, wakanywa na kufurahi.

  15. Mfalme Solomoni akatawala katika falme zote kuanzia Mto Frati hadi nchi ya Wafilisti, hadi kwenye mpaka wa Misri. Nchi hizi zilileta ushuru na zilikuwa chini ya Solomoni, siku zote za maisha yake.

  16. Mahitaji ya Solomoni ya kila siku yalikuwa kori thelathini za unga laini, kori sitini za unga wa kawaida.

  17. Ngʼombe kumi wa zizini, ngʼombe ishirini wa malisho, kondoo na mbuzi mia moja, pamoja na ayala, paa, kulungu na kuku wazuri sana.

  18. Maafisa wa eneo hilo, kila mmoja katika mwezi wake, walileta mahitaji kwa ajili ya Mfalme Solomoni na wote waliokula mezani mwa mfalme. Walihakikisha kuwa hakuna chochote kilichopungua.

  19. Pia walileta sehemu walizopangiwa za shayiri na majani kwa ajili ya farasi wavutao magari na farasi wengine mahali palipostahili.