Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Self-Righteousness

195 mistari · 30 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Wakaja kama kikundi kuwapinga Mose na Aroni, wakawaambia, “Ninyi mmejitukuza sana! Kusanyiko hili lote ni takatifu, kila mmoja wao, naye Bwana yu pamoja nao. Kwa nini basi mmejitukuza wenyewe juu ya kusanyiko la Bwana?”

  2. Baada ya Bwana Mungu wenu kuwafukuza mbele yenu, msiseme mioyoni mwenu, “Bwana ametuleta hapa kuimiliki nchi hii kwa sababu ya haki yetu.” La, ni kwa sababu ya uovu wa mataifa haya ndiyo Bwana anawafukuza mbele yenu.

  3. Si kwa sababu ya haki yenu wala uadilifu wenu kwamba mtaimiliki nchi yao; lakini kwa sababu ya uovu wa mataifa haya, Bwana Mungu wenu atawafukuza mbele yenu, ili kutimiza lile alilowaapia baba zenu Abrahamu, Isaki na Yakobo.

  4. Basi mjue, si kwa sababu ya haki yenu Bwana Mungu wenu anawapa nchi hii nzuri kuimiliki, kwa kuwa ninyi ni taifa lenye shingo ngumu.

  5. Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake, lakini waovu watanyamazishwa kwenye giza. “Si kwa nguvu mtu hushinda;

  6. Samweli alipomfikia, Sauli akamwambia, “Bwana akubariki! Nimetimiza yale Bwana aliniagiza.”

  7. Je, ninao uwezo wowote wa kujisaidia mimi mwenyewe, wakati ambapo mafanikio yamefukuziwa mbali nami?

  8. Hata kama sikuwa na hatia, kinywa changu kingenihukumu; kama sikuwa na kosa, kingenitangaza kuwa mwenye hatia.

  9. Hata kama ningejiosha kwa sabuni na kutakasa mikono yangu kwa magadi,

  10. wewe ungenitupa kwenye shimo la utelezi kiasi kwamba hata nguo zangu zingenichukia sana.

  11. Unamwambia Mungu, ‘Imani yangu ni kamili nami ni safi mbele zako.’

  12. Aha! Laiti kwamba Mungu angesema, kwamba angefungua midomo yake dhidi yako,

  13. naye akufunulie siri za hekima, kwa kuwa hekima ya kweli ina pande mbili. Ujue hili: Mungu amesahau hata baadhi ya dhambi zako.

  14. “Bila shaka ninyi ndio watu, nayo hekima itakoma mtakapokufa!

  15. Lakini ninayo shauku ya kuzungumza na Mwenyezi na kuhojiana shauri langu na Mungu.

  16. “Nyamazeni kimya nipate kusema; kisha na yanipate yatakayonipata.

  17. Ingawa ataniua, bado nitamtumaini; hakika nitazitetea njia zangu mbele zake.

  18. Sasa kwamba nimekwisha kutayarisha mambo yangu, ninajua mimi nitahesabiwa kuwa na haki.

  19. Je, kuna yeyote anayeweza kuleta mashtaka dhidi yangu? Kama ndivyo, nitanyamaza kimya na nife.

  20. Hata hivyo mikono yangu haijafanya jeuri, na maombi yangu ni safi.

  21. “Ee nchi, usiifunike damu yangu, nacho kilio changu kisinyamazishwe kamwe.

  22. “Je, ni lini utafika mwisho wa maneno haya? Uwe mwenye busara, nasi ndipo tutakapoweza kuongea.

  23. Kwa nini sisi tunafikiriwa kama wanyama, na kuonekana wajinga machoni pako?

  24. Wewe unayejirarua mwenyewe vipande vipande katika hasira yako, je, dunia iachwe kwa ajili yako wewe? Au ni lazima miamba iondolewe mahali pake?

  25. “Ninayajua kikamilifu yale mnayoyafikiri, mipango ambayo kwayo mngenitendea mabaya.