Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Rain: Forty days of, at the time of the flood

12 mistari · 65 vipengele

Mistari kuhusu Forty days of, at the time of the flood

  1. Siku saba kuanzia sasa nitaleta mvua juu ya nchi kwa siku arobaini usiku na mchana, nami nitafutilia mbali kutoka uso wa nchi kila kiumbe hai nilichokiumba.”

  2. Baada ya siku saba, maji ya gharika yakaja juu ya dunia.

  3. Katika siku ya kumi na saba ya mwezi wa pili mwaka wa 600 wa kuishi kwake Noa, siku hiyo ndipo chemchemi zote hata zilizo chini sana ya ardhi zilibubujika kwa nguvu, na malango ya mafuriko ya mbinguni yakafunguliwa.

  4. Mvua ikanyesha juu ya nchi siku arobaini usiku na mchana.

  5. Kwa siku arobaini mafuriko yaliendelea kujaa duniani na maji yalivyozidi kuongezeka, yaliinua safina juu sana kutoka kwenye uso wa nchi.

  6. Maji yakajaa na kuongezeka sana juu ya nchi, na safina ikaelea juu ya uso wa maji.

  7. Maji yakazidi kujaa juu ya nchi, yakaifunika milima yote mirefu chini ya mbingu yote.

  8. Maji yakaendelea kujaa yakaifunika milima kwa kina cha zaidi ya dhiraa kumi na tano.

  9. Kila kiumbe hai kitambaacho juu ya nchi kikaangamia: Ndege, wanyama wa kufugwa, wanyama pori, viumbe vyote juu ya nchi na wanadamu wote.

  10. Kila kiumbe juu ya nchi kavu chenye pumzi ya uhai kikafa.

  11. Kila kitu chenye uhai juu ya uso wa nchi kilifutiliwa mbali, watu, wanyama, viumbe vitambaavyo na ndege warukao angani wakafutiliwa mbali toka duniani. Waliobaki ni Noa peke yake na wale waliokuwa pamoja naye ndani ya safina.

  12. Maji yakaifunika dunia kwa siku 150.