Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Oppression

86 mistari · 8 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Sasa kilio cha Waisraeli kimenifikia, nami nimeona jinsi Wamisri wanavyowatesa.

  2. “Usimtendee mgeni vibaya au kumwonea, kwa kuwa nanyi mlikuwa wageni huko Misri.

  3. “Usimdhulumu mjane wala yatima.

  4. Kama ukifanya hivyo nao wakinililia, hakika nitasikia kilio chao.

  5. Hasira yangu itawaka, nami nitawaua kwa upanga, wake zenu watakuwa wajane na watoto wenu watakuwa yatima.

  6. Ikiwa mtumwa amekimbilia kwako, usimrudishe kwa bwana wake.

  7. Mwache aishi miongoni mwenu mahali popote anapopapenda na katika mji wowote anaochagua. Usimwonee.

  8. Usimwonee mtu maskini na mhitaji ambaye umemwajiri, akiwa ni nduguyo Mwisraeli au mgeni anayeishi katika mojawapo ya miji yenu.

  9. Mlipe ujira wake kila siku kabla ya jua kutua, kwa sababu yeye ni maskini na anautegemea ujira huo. La sivyo, anaweza kumlilia Bwana dhidi yako, nawe ukapata hatia ya dhambi.

  10. Kisha tulimlilia Bwana, Mungu wa baba zetu, naye Bwana akasikia sauti yetu na akaona huzuni yetu, taabu yetu na mateso yetu.

  11. Hivyo hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia mikononi mwa wavamizi waliowateka nyara. Akawauza katika mikono ya adui zao pande zote, hivyo hawakuweza tena kuwazuia adui zao.

  12. akafuata shauri la vijana wa rika lake na kusema, “Baba yangu alifanya nira yenu kuwa nzito, mimi nitaifanya kuwa nzito zaidi. Baba yangu aliwachapa kwa mijeledi, mimi nitawachapa kwa nge.”

  13. “Hili ndilo fungu ambalo Mungu humpa mtu mwovu, urithi ule mtu mdhalimu anapokea kutoka kwa Mwenyezi:

  14. Hata kama watoto wake watakuwa wengi kiasi gani, fungu lao ni kuuawa kwa upanga; wazao wake hawatakuwa kamwe na chakula cha kuwatosha.

  15. Tauni itawazika wale watakaonusurika miongoni mwao, nao wajane wao hawatawaombolezea.

  16. Ajapokusanya fedha nyingi kama mavumbi, na mavazi kama malundo ya udongo wa mfinyanzi,

  17. yale yote mtu mwovu aliyojiwekea akiba, mwenye haki atayavaa, naye asiye na hatia ataigawanya fedha yake.

  18. Nyumba aijengayo ni kama utando wa buibui, kama kibanda alichotengeneza mlinzi.

  19. Yeye hulala akiwa tajiri, lakini ndiyo mara ya mwisho; afunguapo macho yake, yote yametoweka.

  20. Vitisho humjia kama mafuriko; dhoruba humkumba ghafula usiku.

  21. Upepo mkali wa mashariki humchukua, naye hutoweka; humzoa kutoka mahali pake.

  22. Humvurumisha bila huruma, huku akikimbia kasi kukwepa nguvu zake.

  23. Upepo humpigia makofi kwa dharau, na kumfukuza atoke mahali pake.

  24. Bwana ni kimbilio la watu wanaoonewa, ni ngome imara wakati wa shida.

  25. Unasikia, Ee Bwana, shauku ya wanaoonewa, wewe huwatia moyo, na kusikiliza kilio chao,