Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Martyrdom

58 mistari · 20 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu wako na manabii wako, nawe umewapa damu wanywe kama walivyostahili.”

  2. Nikaona kuwa huyo mwanamke alikuwa amelewa kwa damu ya watakatifu, yaani, damu ya wale watu waliouawa kwa ushuhuda wa Yesu. Nilipomwona huyo mwanamke, nilistaajabu sana.

  3. Furahia kwa ajili yake, ee mbingu! Furahini watakatifu, mitume na manabii! Mungu amemhukumu kwa vile alivyowatendea ninyi.’ ”

  4. Kisha malaika mmoja mwenye nguvu akainua jiwe kubwa kama la kusagia akalitupa baharini akisema: “Hivyo ndivyo mji mkubwa Babeli utakavyotupwa chini kwa nguvu wala hautaonekana tena.

  5. Nyimbo za wapiga vinubi na waimbaji, wapiga filimbi na wapiga tarumbeta kamwe hazitasikika tena ndani yako. Ndani yako kamwe hataonekana tena fundi mwenye ujuzi wa aina yoyote. Wala sauti ya jiwe la kusagia kamwe haitasikika tena.

  6. Mwanga wa taa hautaangaza ndani yako tena. Sauti ya bwana arusi na bibi arusi kamwe haitasikika ndani yako tena. Wafanyabiashara wako walikuwa watu maarufu wa dunia. Mataifa yote yalipotoshwa kwa uchawi wako.

  7. Ndani yake ilionekana damu ya manabii na ya watakatifu na wote waliouawa duniani.”

  8. Kisha nikaona viti vya enzi vilivyokuwa vimekaliwa na hao waliopewa mamlaka ya kuhukumu, na nikaona roho za wale waliokatwa vichwa kwa sababu ya ushuhuda wa Yesu na kwa sababu ya neno la Mungu. Hawakuwa wamemsujudu huyo mnyama wala sanamu yake wala hawakupokea ile chapa yake kwenye vipaji vya nyuso zao au kwenye mikono yao. Wakawa hai na kutawala pamoja na Kristo miaka 1,000.