Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Humility

90 mistari · 43 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Ndipo Mfalme Daudi akaingia ndani, akaketi mbele za Bwana, akasema: “Ee Bwana Mwenyezi, mimi ni nani, na jamaa yangu ni nini, hata umenileta mpaka hapa nilipo?

  2. Naam, kana kwamba hili halitoshi machoni pako, Ee Bwana Mwenyezi, wewe umenena pia kuhusu siku zijazo za nyumba ya mtumishi wako. Je, hii ndiyo njia yako ya kawaida ya kushughulika na mwanadamu, Ee Bwana Mwenyezi?

  3. “Mwanadamu ni kitu gani hata umjali kiasi hiki, kwamba unamtia sana maanani,

  4. kwamba unamwangalia kila asubuhi na kumjaribu kila wakati?

  5. “Ni vipi basi mimi nitaweza kubishana naye? Nawezaje kupata maneno ya kuhojiana naye?

  6. Ingawa sikuwa na hatia, sikuweza kumjibu; ningeweza tu kumsihi Mhukumu wangu anihurumie.

  7. Ikiwa hata mwezi sio mwangavu nazo nyota si safi machoni pake,

  8. sembuse mtu ambaye ni funza: mwanadamu ambaye ni buu tu!”

  9. “Mimi sistahili kabisa: ninawezaje kukujibu wewe? Nauweka mkono wangu juu ya kinywa changu.

  10. Nimesema mara moja, lakini sina jibu; naam, nimesema mara mbili, lakini sitasema tena.”

  11. “Ulisema, ‘Sikiliza sasa, nami nitanena; nitakuuliza swali, nawe yakupasa kunijibu.’

  12. Masikio yangu yalikuwa yamesikia habari zako, lakini sasa macho yangu yamekuona.

  13. Kwa hiyo najidharau mwenyewe, na kutubu katika mavumbi na majivu.”

  14. Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, mwezi na nyota, ulizoziratibisha,

  15. mwanadamu ni kitu gani hata unamfikiria, binadamu ni nani hata unamjali?

  16. Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. Moyo wangu hauna kiburi, Ee Bwana, macho yangu hayajivuni; sijishughulishi na mambo makuu kunizidi wala mambo ya ajabu mno kwangu.

  17. Lakini nimetuliza na kunyamazisha nafsi yangu; kama mtoto aliyeachishwa kunyonya na mama yake, kama mtoto aliyeachishwa kunyonya ndivyo ilivyo nafsi iliyoko ndani yangu.

  18. Ee Bwana, mwanadamu ni nini hata umjali, Binadamu ni nini hata umfikirie?

  19. Mwanadamu ni kama pumzi, siku zake ni kama kivuli kinachopita.

  20. Usijikweze mwenyewe mbele ya mfalme, wala usidai nafasi miongoni mwa watu wakuu;

  21. ni afadhali yeye akuambie, “Njoo huku juu,” kuliko yeye kukuaibisha mbele ya mkuu. Kile ulichokiona kwa macho yako

  22. “Mimi ni mjinga kuliko wanadamu wote; sina ufahamu wa kibinadamu.

  23. Sijajifunza hekima, wala sina maarifa ya kumjua yeye Aliye Mtakatifu.

  24. Ninajua, Ee Bwana, kwamba maisha ya mwanadamu si yake mwenyewe; hawezi kuziongoza hatua zake mwenyewe.

  25. Unirudi, Ee Bwana, lakini kwa kipimo cha haki: si katika hasira yako, usije ukaniangamiza.