Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Drunkenness

52 mistari · 31 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Watawaambia wazee, “Huyu mwanetu ni mkaidi na mwasi. Hatutii sisi, yeye ni mpotovu na mlevi.”

  2. Kisha wanaume wote wa mjini mwake watampiga kwa mawe mpaka afe. Ndivyo imewapasa kuondoa maovu kati yenu. Israeli yote itasikia hili na kuogopa.

  3. Wakati mtu wa namna hii asikiapo maneno ya kiapo hiki, hujibariki mwenyewe na kisha hufikiri, “Nitakuwa salama, hata kama nikiendelea kuifuata njia yangu mwenyewe.” Hili litaleta maafa juu ya nchi iliyonyeshewa sawasawa na nchi kame.

  4. Bwana kamwe hatakuwa radhi kumsamehe, ghadhabu na wivu wa Mungu vitawaka dhidi ya mtu huyo. Laana zote zilizoandikwa katika kitabu hiki zitamwangukia na Bwana atafuta jina lake chini ya mbingu.

  5. Bwana atamtwaa peke yake kutoka makabila ya Israeli kwa maangamizo, kulingana na laana zote za Agano zilizoandikwa kwenye Kitabu hiki cha Sheria.

  6. Usiwe miongoni mwa wanywao mvinyo, au wale walao nyama kwa pupa,

  7. kwa maana walevi na walafi huwa maskini, nako kusinzia huwavika matambara.

  8. Ni nani mwenye ole? Ni nani mwenye huzuni? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye malalamiko? Ni nani aliye na majeraha yasiyo na sababu? Ni nani mwenye macho mekundu?

  9. Ni hao wakaao sana kwenye mvinyo, hao waendao kuonja mabakuli ya mvinyo uliochanganywa.

  10. Usiukodolee macho mvinyo wakati ukiwa mwekundu, wakati unapometameta kwenye bilauri, wakati ushukapo taratibu!

  11. Mwishowe huuma kama nyoka na kutia sumu yake kama nyoka mwenye sumu.

  12. Macho yako yataona mambo mageni na moyo wako kuwazia mambo yaliyopotoka.

  13. Utakuwa kama alalaye katikati ya bahari, alalaye juu ya kamba ya merikebu.

  14. Utasema, “Wamenipiga lakini sikuumia! Wamenichapa, lakini sisikii! Nitaamka lini ili nikanywe tena?”

  15. “Ee Lemueli, haifai wafalme, haifai wafalme kunywa mvinyo, haifai watawala kutamani sana kileo,

  16. wasije wakanywa na kusahau vile sheria inavyoamuru na kuwanyima haki zao wote walioonewa.

  17. Wape kileo wale wanaoangamia, mvinyo wale walio na uchungu,

  18. Wanywe na kusahau umaskini wao na wasikumbuke taabu yao tena.

  19. Ole wao wale waamkao asubuhi na mapema wakikimbilia kunywa vileo, wale wakawiao sana mpaka usiku, mpaka wamewaka kwa mvinyo.

  20. Wana vinubi na zeze kwenye karamu zao, matari, filimbi na mvinyo, lakini hawayajali matendo ya Bwana, wala hawana heshima kwa ajili ya kazi ya mikono yake.

  21. Ole kwa lile taji la maua, kiburi cha walevi wa Efraimu, kwa ua linalosinyaa, uzuri wa utukufu wake, uliowekwa kwenye kichwa cha bonde lenye rutuba: kwa ule mji, kiburi cha wale walioshushwa na mvinyo!

  22. Tazama, Bwana anaye mmoja aliye na uwezo na nguvu. Kama dhoruba ya mvua ya mawe na upepo uharibuo, kama mvua inyeshayo kwa nguvu na mafuriko yashukayo, atakiangusha chini kwa nguvu.

  23. Lile taji la maua, kiburi cha walevi cha Efraimu, kitakanyagwa chini ya nyayo.

  24. Hawa pia wanapepesuka kwa sababu ya mvinyo, wanayumbayumba kwa sababu ya kileo: Makuhani na manabii wanapepesuka kwa sababu ya kileo, wanachanganyikiwa kwa sababu ya mvinyo; wanapepesuka wanapoona maono, wanajikwaa wanapotoa maamuzi.

  25. Meza zote zimejawa na matapishi wala hakuna sehemu hata ndogo isiyokuwa na uchafu.