Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Church (2): Love for

18 mistari · 7 vipengele

Mistari kuhusu Love for

  1. Bwana na akubariki kutoka Sayuni siku zote za maisha yako, na uone mafanikio ya Yerusalemu,

  2. nawe ujaliwe kuishi uone watoto wa watoto wako. Amani iwe juu ya Israeli.

  3. Kando ya mito ya Babeli tuliketi, tukaomboleza tulipokumbuka Sayuni.

  4. Kwenye miti ya huko tulitundika vinubi vyetu,

  5. kwa maana huko hao waliotuteka walitaka tuwaimbie nyimbo, watesi wetu walidai nyimbo za furaha; walisema, “Tuimbieni wimbo mmoja kati ya nyimbo za Sayuni!”

  6. Tutaimbaje nyimbo za Bwana, tukiwa nchi ya kigeni?

  7. Nikikusahau wewe, ee Yerusalemu, basi mkono wangu wa kuume na usahau ujuzi wake.

  8. Ulimi wangu ushikamane na kaakaa la kinywa changu kama sitakukumbuka wewe, kama nisipokufikiri Yerusalemu kuwa furaha yangu kubwa.

  9. Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, ee Yerusalemu, hawatanyamaza mchana wala usiku. Ninyi wenye kumwita Bwana, msitulie,

  10. msimwache apumzike hadi atakapoufanya imara Yerusalemu na kuufanya uwe sifa ya dunia.

  11. Kama mama anavyomfariji mtoto wake, ndivyo nitakavyokufariji wewe, nawe utafarijiwa huko Yerusalemu.”

  12. Wakati mtakapoona jambo hili, mioyo yenu itashangilia, nanyi mtastawi kama majani; mkono wa Bwana utajulikana kwa watumishi wake, bali ghadhabu yake kali itaonyeshwa kwa adui zake.

  13. Wewe uliyepona upanga, ondoka wala usikawie! Mkumbuke Bwana ukiwa katika nchi ya mbali, na utafakari juu ya Yerusalemu.”

  14. “Tumetahayari, kwa maana tumetukanwa na aibu imefunika nyuso zetu, kwa sababu wageni wameingia mahali patakatifu pa nyumba ya Bwana.”

  15. Vijito vya machozi vinatiririka kutoka machoni mwangu, kwa sababu watu wangu wameangamizwa.

  16. Macho yangu yatatiririka machozi bila kukoma, bila kupata nafuu,

  17. hadi Bwana atazame chini kutoka mbinguni na kuona.

  18. Lile ninaloliona huniletea huzuni nafsini kwa sababu ya wanawake wote wa mji wangu.