Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Church (2)

158 mistari · 7 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Kuna mto ambao vijito vyake vinaufurahisha mji wa Mungu, mahali patakatifu ambako Aliye Juu Sana anaishi.

  2. Mungu yuko katikati yake, hautaanguka, Mungu atausaidia asubuhi na mapema.

  3. Wimbo. Zaburi ya wana wa Kora. Bwana ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana, katika mji wa Mungu wetu, mlima wake mtakatifu.

  4. Ni mzuri katika kuinuka kwake juu sana, furaha ya dunia yote. Kama vilele vya juu sana vya Safoni ni Mlima Sayuni, mji wa Mfalme Mkuu.

  5. Mlima Sayuni unashangilia, vijiji vya Yuda vinafurahi kwa sababu ya hukumu zako.

  6. Tembeeni katika Sayuni, uzungukeni mji, hesabuni minara yake;

  7. yatafakarini vyema maboma yake, angalieni ngome zake, ili mpate kusimulia habari zake kwa kizazi kijacho.

  8. kwa maana Mungu ataiokoa Sayuni na kuijenga tena miji ya Yuda. Kisha watu watafanya makao yao humo na kuimiliki,

  9. watoto wa watumishi wake watairithi na wale wote walipendao jina lake wataishi humo.

  10. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa gitithi. Zaburi ya wana wa Kora. Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, makao yako yapendeza kama nini!

  11. Nafsi yangu inatamani sana, naam, hata kuona shauku, kwa ajili ya nyua za Bwana; moyo wangu na mwili wangu vinamlilia Mungu Aliye Hai.

  12. Hata shomoro amejipatia makao, mbayuwayu amejipatia kiota mahali awezapo kuweka makinda yake: mahali karibu na madhabahu yako, Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mfalme wangu na Mungu wangu.

  13. Heri wale wanaokaa nyumbani mwako, wanaokusifu wewe daima.

  14. Heri wale ambao nguvu zao ziko kwako, na njia ziendazo Sayuni zimo mioyoni mwao.

  15. Wanapopita katika Bonde la Baka, hulifanya mahali pa chemchemi, pia mvua za vuli hulijaza kwa madimbwi.

  16. Huendelea toka nguvu hadi nguvu, hadi kila mmoja afikapo mbele za Mungu huko Sayuni.

  17. Ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, sikia maombi yangu; nisikilize, Ee Mungu wa Yakobo.

  18. Ee Mungu, uitazame ngao yetu, mtazame kwa wema mpakwa mafuta wako.

  19. Siku moja katika nyua zako ni bora kuliko siku elfu mahali pengine; afadhali ningekuwa bawabu katika nyumba ya Mungu wangu kuliko kukaa katika mahema ya waovu.

  20. Zaburi ya wana wa Kora. Wimbo. Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu;

  21. Bwana anayapenda malango ya Sayuni kuliko makao yote ya Yakobo.

  22. Mambo matukufu yanasemwa juu yako, ee mji wa Mungu:

  23. “Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu na Babeli miongoni mwa wale wanaonikubali mimi: Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi, nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’ ”

  24. Kuhusu Sayuni itasemwa hivi, “Huyu na yule walizaliwa humo, naye Aliye Juu Sana mwenyewe atamwimarisha.”

  25. Bwana ataandika katika orodha ya mataifa: “Huyu alizaliwa Sayuni.”