Rukia maudhui

circa 6 BC – AD 30

The Life of Jesus

The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.

3,779 mistari · 4 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Yohana 3:25takriban 30 BK

    Mashindano yakazuka kati ya baadhi ya wanafunzi wa Yohana na Myahudi mmoja kuhusu suala la desturi ya kunawa kwa utakaso.

  2. Yohana 3:26takriban 30 BK

    Wakamwendea Yohana wakamwambia, “Rabi, yule mtu aliyekuwa pamoja nawe ngʼambo ya Mto Yordani, yule uliyeshuhudia habari zake, sasa anabatiza na kila mtu anamwendea!”

  3. Yohana 3:27takriban 30 BK

    Yohana akawajibu, “Hakuna mtu yeyote awezaye kupata kitu chochote isipokuwa kile tu alichopewa kutoka mbinguni.

  4. Yohana 3:28takriban 30 BK

    Ninyi wenyewe ni mashahidi wangu kwamba nilisema, ‘Mimi si Kristo, ila nimetumwa nimtangulie.’

  5. Yohana 3:29takriban 30 BK

    Bibi arusi ni wa bwana arusi. Lakini rafiki yake bwana arusi anayesimama karibu naye na kusikiliza kutoka kwake, hufurahi sana aisikiapo sauti ya bwana arusi. Kwa sababu hii furaha yangu imekamilika.

  6. Yohana 3:30takriban 30 BK

    Yeye hana budi kuwa mkuu zaidi na mimi nizidi kuwa mdogo.”

  7. Yohana 3:31takriban 30 BK

    “Yeye ajaye kutoka juu yu juu ya yote, yeye aliye wa duniani ni wa dunia, naye huzungumza mambo ya duniani. Yeye aliyekuja kutoka mbinguni, yu juu ya yote.

  8. Yohana 3:32takriban 30 BK

    Yeye hushuhudia yale aliyoyaona na kuyasikia, lakini hakuna yeyote anayekubali ushuhuda wake.

  9. Yohana 3:33takriban 30 BK

    Lakini yeyote anayekubali huo ushuhuda anathibitisha kwamba, Mungu ni kweli.

  10. Yohana 3:34takriban 30 BK

    Yeye aliyetumwa na Mungu husema maneno ya Mungu, kwa kuwa Mungu humtoa Roho pasipo kipimo.

  11. Yohana 3:35takriban 30 BK

    Baba anampenda Mwana, naye ametia vitu vyote mikononi mwake.

  12. Yohana 3:36takriban 30 BK

    Yeyote anayemwamini Mwana ana uzima wa milele, lakini yeye asiyemwamini Mwana hatauona uzima, bali ghadhabu ya Mungu itakuwa juu yake.”

  13. Yohana 4:1takriban 30 BK

    Mafarisayo wakasikia kwamba Yesu alikuwa anapata na kubatiza wanafunzi wengi zaidi kuliko Yohana,

  14. Yohana 4:2takriban 30 BK

    ingawa kwa kweli si Yesu mwenyewe aliyekuwa akibatiza, ila ni wanafunzi wake.

  15. Yohana 4:3takriban 30 BK

    Bwana alipojua mambo haya, aliondoka Uyahudi akarudi tena Galilaya.

  16. Yohana 4:4takriban 30 BK

    Wakati huo ilimlazimu apitie Samaria.

  17. Yohana 4:5takriban 30 BK

    Akafika kwenye mji mmoja wa Samaria uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa mwanawe Yosefu.

  18. Yohana 4:6takriban 30 BK

    Huko ndiko kulikokuwa na kile kisima cha Yakobo. Naye Yesu alikuwa amechoka kwa kuwa alikuwa ametoka safarini. Akaketi karibu na hicho kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana.

  19. Yohana 4:7takriban 30 BK

    Mwanamke mmoja Msamaria akaja kuteka maji, Yesu akamwambia, “Naomba maji ninywe.”

  20. Yohana 4:8takriban 30 BK

    (Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wamekwenda mjini kununua chakula.)

  21. Yohana 4:9takriban 30 BK

    Yule mwanamke Msamaria akamjibu, “Wewe ni Myahudi na mimi ni Msamaria. Yawezekanaje uniombe nikupe maji ya kunywa?” (Wayahudi walikuwa hawashirikiani kabisa na Wasamaria.)

  22. Yohana 4:10takriban 30 BK

    Yesu akajibu akamwambia, “Kama ungelijua karama ya Mungu, naye ni nani anayekuambia, Nipe maji ninywe, wewe ungelimwomba yeye, naye angelikupa maji yaliyo hai.”

  23. Yohana 4:11takriban 30 BK

    Yule mwanamke akamjibu, “Bwana, wewe huna chombo cha kutekea maji na kisima hiki ni kirefu. Hayo maji ya uzima utayapata wapi?

  24. Yohana 4:12takriban 30 BK

    Kwani wewe ni mkuu kuliko baba yetu Yakobo ambaye alitupatia kisima hiki, ambacho yeye pamoja na watoto wake na mifugo yake walikitumia?”

  25. Yohana 4:13takriban 30 BK

    Yesu akamjibu, “Kila mtu anayekunywa maji ya kisima hiki ataona kiu tena.