circa 6 BC – AD 30
The Life of Jesus
The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.
Mistari ya kipindi hiki
- Yohana 4:14takriban 30 BK
Lakini yeyote anywaye maji nitakayompa hataona kiu kamwe. Maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujika uzima wa milele.”
- Yohana 4:15takriban 30 BK
Yule mwanamke akamwambia, “Bwana, tafadhali nipe maji hayo ili nisipate kiu tena na wala nisije tena hapa kuteka maji!”
- Yohana 4:16takriban 30 BK
Yesu akamjibu, “Nenda ukamwite mumeo, uje naye hapa.”
- Yohana 4:17takriban 30 BK
Yule mwanamke akajibu, “Sina mume.” Yesu akamwambia, “Umesema kweli kuwa huna mume.
- Yohana 4:18takriban 30 BK
Kwa maana umeshakuwa na wanaume watano na mwanaume unayeishi naye sasa si mume wako! Umesema ukweli.”
- Yohana 4:19takriban 30 BK
Yule mwanamke akasema, “Bwana, naona bila shaka wewe ni nabii.
- Yohana 4:20takriban 30 BK
Baba zetu waliabudu kwenye mlima huu, lakini ninyi Wayahudi mnasema ni lazima tukaabudu huko Yerusalemu.”
- Yohana 4:21takriban 30 BK
Yesu akamjibu, “Mwanamke, niamini, wakati unakuja ambapo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala huko Yerusalemu.
- Yohana 4:22takriban 30 BK
Ninyi Wasamaria mnaabudu msichokijua. Sisi Wayahudi tunamwabudu Mungu tunayemjua kwa sababu wokovu unatoka kwa Wayahudi.
- Yohana 4:23takriban 30 BK
Lakini saa yaja, tena ipo, ambapo wale waabuduo halisi, watamwabudu Baba katika roho na kweli. Watu wanaoabudu namna hii, ndio Baba anawatafuta.
- Yohana 4:24takriban 30 BK
Mungu ni Roho na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.”
- Yohana 4:25takriban 30 BK
Yule mwanamke akamwambia, “Ninafahamu kwamba Masiya (aitwaye Kristo) anakuja. Yeye akija, atatueleza mambo yote.”
- Yohana 4:26takriban 30 BK
Yesu akamwambia, “Mimi ninayezungumza nawe, ndiye.”
- Yohana 4:27takriban 30 BK
Wakati huo wanafunzi wake wakarudi, wakashangaa sana kumwona akizungumza na mwanamke. Lakini hakuna aliyemuuliza, “Unataka nini kwake?” Au “Kwa nini unazungumza naye?”
- Yohana 4:28takriban 30 BK
Yule mwanamke akaacha mtungi wake, akarudi mjini akawaambia watu,
- Yohana 4:29takriban 30 BK
“Njooni mkamwone mtu aliyeniambia kila kitu nilichotenda! Je, yawezekana huyu ndiye Kristo?”
- Yohana 4:30takriban 30 BK
Basi wakamiminika watu kutoka mjini wakamwendea Yesu.
- Yohana 4:31takriban 30 BK
Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wakimsihi, “Rabi, kula angalau chochote.”
- Yohana 4:32takriban 30 BK
Lakini yeye akawajibu, “Mimi ninacho chakula ambacho ninyi hamkifahamu.”
- Yohana 4:33takriban 30 BK
Basi wanafunzi wakaanza kuulizana, “Kuna mtu ambaye amemletea chakula?”
- Yohana 4:34takriban 30 BK
Lakini Yesu akawajibu, “Chakula changu ni kufanya mapenzi ya Mungu ambaye amenituma na kuikamilisha kazi yake.
- Yohana 4:35takriban 30 BK
Je, ninyi hamsemi, ‘Bado miezi minne tuvune?’ Inueni macho yenu myaangalie mashamba jinsi mazao yalivyo tayari kuvunwa!
- Yohana 4:36takriban 30 BK
Mvunaji tayari anapokea mshahara wake, naye anakusanya mazao kwa ajili ya uzima wa milele. Ili yeye apandaye na yeye avunaye wafurahi pamoja.
- Yohana 4:37takriban 30 BK
Hivyo kule kusema, ‘Mmoja hupanda na mwingine huvuna,’ ni kweli kabisa.
- Yohana 4:38takriban 30 BK
Niliwatuma mkavune mazao ambayo hamkupanda, wengine walifanya kazi ngumu, nanyi mmevuna faida ya taabu yao.”